Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (aliyesimama), akizungumza na watumshi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, (hawapo pichani), katika hafla ya kuagana iliyofanyika katika ukumbi wa ‘Golden Crown’ Jijini Dodoma, mara baada ya kukamilisha Tamasha la Pasaka lilioambatana na Bonanza la michezo na kukamilishwa na matendo ya huruma kwa kutembelea na kugawa misaada ya vyakula, fedha, na mahitaji mengine katika vituo mbali mbali vya watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo kituo cha Safina, Asmaa Bint Shams kilichopo kisasa, kituo cha wasiooa watu wazima Buigiri na kituo cha watoto wenye uhitaji maalum Shule ya Msingi Buigiri.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (kulia), akiteta jambo na Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, katika hafla ya kuagana Watumishi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango – Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa ‘Golden Crown’ Jijini Dodoma.
Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, (aliyesimama), akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea vituo vya watu wenye mahitaji maalum, na Watoto yatima jijini Dodoma, kama sehemu ya matendo ya huruma yaliyoambatana na kugawa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula, dawa za meno, vinywaji, fedha na mahitaji mengine muhimu kwa niaba ya Watumishi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kukamilisha Tamasha la Pasaka linalofanyika kila mwaka.
Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, (wapili kushoto), akikabidhi moja ya zawadi kwa Watoto wenye mahitaji maalum, wanaolelewa katika kituo cha Safina Jijini Dodoma, kwa niaba ya wafayakazi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar walipotembelea katika vituo hivyo na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo fedha, vyakula, vinywaji na mahitaji mengine muhimu kama sehemu ya kukamilisha Tamasha la Pasaka mwaka 2024.
Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka ambaye pia ni Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bw. Mgusi Musifa, (wakwanza kushoto), pamoja na Afisa Uendeshaji, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, (wapili kushoto) wakimkabidhi Mwenyekiti wa Kituo cha Makazi ya wasioona cha Matembebora, kilichopo Buigiri Jijini Dodoma Bw. Yarid Daud Chereso, sehemu ya msaada uliyotolewa na Watumishi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.
Picha za Matukio mbali mbali ya watoto wanaolelewa katika vituo vya kulelea Watoto yatima na watu wenye uhitaji maalum Jijini Dodoma, wakiomba dua na kufanya maombi maalum baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, katika vituo vyao na kupewa misaada mbalimbali ikiwemo vyakula, vinywaji, fedha na mahitaji mengine.
Picha za Matukio mbali mbali katika hafla ya kuagana kati ya Watumishi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Watumishi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Golden Croun Jijini Dodoma mara baada ya kukamilisha ratiba ya kutembelea vituo vya watu wenye uhitaji maalum ikiwemo Watoto yatima na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo fedha, vyakula vinywaji, na mahitaji mengine muhimu.
………………..
Na Asia Singano na Chedaiwe Msuya – WF- Dodoma
Tamasha la Pasaka lililoandaliwa na Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na MipangoZanzibar kwa Mwaka 2024, limehitimishwa baada ya watumishi wa Wizara ya Fedha pande zote mbili za Muungano kukamilisha zoezi la kutoa misaada kwa vituo mbalimbali vya watu wenye uhitaji maalum na vituo vya watoto yatima.
Akizungumza katika hafla ya kuagana na Watumishi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa’ Golden Crown’ jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, aliwashukuru watumishi wote wa pande zote mbili kwa ushiriki wao katika Tamasha hilo huku akiahidi kufanyika kwa tukio kama hilo mwakani.
“Nimefurahi sana na nawashukuru kwa ushiriki wenu, msafiri salama na endapo kutakuwa na changamoto yoyote tunaomba mtufahamishe, tuna ofisi sehemu mbalimbali ikiwemo Dar Es Salaam na maeneo mengine hapa nchini hivyo ni rahisi kusaidia ikiwa kutatokea changamoto yoyote ‘’ Alisema Bw. Mwenda
Kwa upande wake, Afisa Uendeshaji kutoka Ofisi ya Raisi Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, akizungumzia kuhusu ziara ya kutembelea vituo vya watu wenye uhitaji, aliainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye mahitaji maalum na vituo vya kulelea watoto yatima ikiwemo makazi na fedha za kujiendesha.
‘’Tumeona changamoto nyingi za vituo hivi mfano kituo cha Safina kina uhitaji wa pampu za kusukuma maji ambazo matengenezo yote yanagharimu kiasi cha shilingi milioni saba na nusu na tumewapa milioni moja tu’’ alisema Bw. Uweje
Aliongeza kuwa Ofisi ya Rais Fedha na Mipago Zanzibar itashirikiana na Wizara ya Fedha Tanzania Bara ili kuona namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye mahitaji maalumu katika vituo hivyo katika awamu nyingine.
“Na tumetoa ahadi kuwa tumechukua zile changamoto zao ili tuone tunaenda kuzifanyia kazi vipi, endapo tutafanikiwa kuwa mshawishi viongozi wetu katika Taasisi zetu basi tutarudi na kuona tutawasaidia vipi”Aliongeza Bw. Uweje.
Aidha, alitoa wito kwa walezi wanaohudumia watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo Watoto yatima kuwalea katika malezi bora ili wasione utofauti na watu wengine ikiwa ni pamoja na kuwasimamia katika masomo yao na kuwapa misingi bora ya kiimani kwa kila mmoja kutokana na dini yake.
“Wito wangu kwa walezi wa vituo waendelee kuwatunza watoto hawa, kuwasimamia vizuri ili muwe na mchango bora kwa Taifa na raia wema wa leo na baadae” alisisitiza Bw. Uweje.
Kila mwaka Watumishi wa Wizara ya Fedha na Watumishi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar hutembelea vituo mbalimbali na kufanya matendo ya huruma katika maeneo yote mawili kwa zamu (Tanzania Bara na Zanzibar) ambapo kwa mwaka huu wametembelea Vituo vya Safina, Asmaa Bint Shams kilichopo kisasa, kituo cha watu wazima (wakubwa) wasioona Buigiri na Kituo cha Watoto wenye uhitaji maalum kilichopo Shule ya Msingi Buigiri na kutoa misaada ya vitu mbalimbai ikiwemo vyakula, sabuni, mafuta, dawa za meno, fedha na mahitaji mengine.