Takribani wachezaji 56 wa mchezo wa Drafti wamechuana vikali katika mashindano ya Drafti ya Mbunge wa Njombe Mjini Deo Mwanyika Mwanyika Draft Cup na kisha Jonas Mwalongo kuibuka Bingwa wa Mashindano hayo kwa mwaka wa Pili Mfululizo na kunyakulia fedha taslimu laki mbili kwa kumchapa mwana fainali mwezie Said Hamis bao mbili kwa sifuri ambae amekabidhiwa shilingi laki moja kwa kumaliza nafasi ya pili katika mashindano hayo.
Wakati akihitimisha mashindano ya Mwanyika Draft Cup ambayo yamechezwa kwa zaidi ya wiki mbili mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika amesema ameongeza bajeti hadi kufika mil 1,60000 ili kuongeza ushindani katika mashindano hayo yanayotumia akili zaidi duniani na kisha kutoa ahadi ya kuanzisha Mwanyika Boxingi,Mshindano ya Pool table ili kuendelea kufua vipaji vya vijana na kuwaepusha na vitendo vya kialifu
Mwanyika amesema anakusudio la kutengeneza timu kali ya Drafti ya mkoa wa Njombe na kisha kufadhili mashindano yatakayohusisha mikoa ya nyanda za juu kusini huku pia akisema kwa kuwa mpira wa miguu ndiyo mpira maarufu ulimwenguni hivyo kupitia Hillside Hotel amekubali kuwa mdhamini wa timu ya mpira wa miguu ya Housing FC ya mkoa wa Njombe ambayo ilicheza na Yanga katika mchezo wa FA siku chache zilizopita.
Ili kuimarisha mchezo wa drafu pia mwanzilishi wa mashindano ya Drafti ambayo yanaingia mwaka wa tatu sasa mbunge huyo wa Njombe Mjini amesema atakwenda kusaidia kifedha usajili wa chama cha Drafti na kisha kuanza mpango wa kuandaa eneo la Mashindano.
Suala lingine ambalo limetolewa ufafanuzi na mbunge wa Njombe mjini ni kuhusu kiu kubwa ya wafuasi wa soka wa mkoa wa Njombe ya kushuhudia mchezo utakaohusisha bingwa kutoka ligi ya mbunge wa jimbo la Lupembe Swale Cup na Bingwa wa jimbo la Njombe Mjini Mwanyika Cup ambapo amesema mapema baada ya kurejea bungeni waratibu wataanza maandalizi ya mchezo huo.
Awali mratibu wa mashindano hayo Aliko Mahenge amezungumzia maendeleo ya mchezo huo tangu mashindano yalipo anzishwa miaka mitatu iliyopita na kisha kueleza changamoto ya hali ya hewa na mrundikano wa majukumu wa wachezaji unavyosababisha kushindwa kushiriki ipasavyo mashindano na kisha kuweka bayana mpango wao wa maboresho katika msimu ujao.
Kwa upande wao washiriki wa Mwanyika Drafti Cup akiwemo Jonas Mwalongo ambae ni bingwa na Said Haamis Mwanafainali mwingine wanasema mashindano yamezidi kuboreshwa kila kukicha na kwamba uwekezaji mkubwa unaofanyika unawafanya kuongeza ufundi huku pia wakisema mchezo wa fainali ulitawaliwa na akili nyingi na uzoefu.
Ukichana na michezo mbunge mwanyika ametoa zawadi ya tende kwa waislamu walio kwenye mfungo na kisha kuwatakia sikuu njema za pasaka wakristo .