Raisa Said,Tanga
Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Tanga, Dk Frederick Sagamiko kuwasimamisha kazi watumishi watano kutoka katika kituo cha afya cha Mikanjuni kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mama mmoja ambaye alijifungua kwa njia ya upasuaji.
Watumushi hao wanaotuhumiwa kwa uzembe ulisaobaisha mama huyo, Fatma Musa Selemani kuwekewa damu kinyume na utaratibu kitu ambacho kilisababisha kupata mzio na hatimaye kufa.
Alisema kuwa serikali imeamua watumishi hao ambao ni madaktari wawili na wauguzi watatu wasimame kazi hadi hapo tume husika itakapo kamilisha uchunguzi na kubaini makosa yao.
“Taarifa za awali zinasema kuwa kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa anahitaji kuwekewa damu katika wodi ambayo pia alilazwa mama huyo mkazi wa Magaoni ambaye alijifungua mtoto kwa njia ya upasuaji,” alisema Kaji
Aliendelea kuelezwa kuwa kwa kuwa hakukuwepo na umakini wa kuachiana taarifa sahihi uzembe huo ulisababisha muuguzi aliyekuwepo zamu kumuwekea damu mama huyo, jambo ambalo lilisababisha yeye kupata mzio na hatimaye kufariki dunia.
Kaji aliwataja watumishi ambao kuwa ni muuguzi aliyekuwa zamu mchana, Fadhili Ali Hoza, wauuguzi wengine waliokuwepo usiku Restituta Kisendo Deusdedit na Muya Ali Mohamed. Aliwataka madaktari kuwa ni Dk Andrew Eliyasikia Kidee, na k Hamis Mohamed Msanii.
Kwa mujibu wa maelezo mama huyo alilazwa katika kituo hicho tarehe 27 mwezi huu akiwa na uchungu, saa tisa mchana na ambapo alielezwa kupata uchungu pingamizi na hivyo madaktari kulazimika kumzalisha kwa njia ya upasuaji,
Mkuu huyo wa Wilaya alitoa pole kwa wafiwa na kueleza masikitiko yake na ya serikali juu ya kifo hicho na kusema serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan haitavumulia uzembe kama huo ambao alisema umeonekana kuaza kushamiri katiika sehemu mbambali nchini hivi sasa katika vituo mbalimbali.
Aliwaonya watumishi wa afya na kuwataka kuwa makini katika kazi ili kuzuia matukiio kama hayo yayasababishwa na uzembe.
Hata hivo Mume wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Rashid Juma ameomba watu kama hao wanaokuwa wazembe na kusababisha matukio kama hayo wachukuliwe hatua kali kwa sababu bila hivyo uzembe huo utaendelea .