Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) imeridhishwa na maendeleo ya Mradi wa kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mkulazi kilichopo Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Kamati hiyo imetembelea kiwanda cha sukari cha Mkulazi kujionea uhalisia wa maendeleo ambapo pamoja na mambo mengine kamati hiyo imeridhishwa pasi na shaka kwenye tija ambayo imeanza kupatikana ambapo kiwanda kimeanza kuzalisha sukari na tayari ipo Sokoni
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu PIC Vuma Augustino amesema matarajio ya serikali na watanzania ni makubwa kwenye uzalishaji wa sukari pamoja na kuongeza ajira ikiwa ni baada ya kiwanda hicho kukamilika kwa asilimia 98 na kuanza uzalishaji wa majaribio.
“Kiwanda cha sukari cha Mkulazi ni cha kipekee katika uzalishaji wa sukari nyeupe kwa ajili ya matumizi ya viwandani ambayo imekuwa ikiagizwa nchi za nje” amesema Makamu Mwenyekiti PIC
Masha Mshomba Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa NSSF amesema tayari kiwanda kimeanza kuzalisha sukari,kuwafikia walaji na kupungua makali y bei ya Sukari katika miezi ya hivi karibuni
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Mkulazi Dkt. Heridelita Msita amesema kuwa kiwanda hicho kimeanza kazi na amewahakikishia watanzania upatikanaji wa sukari ya kutosha kutoka kwenye kiwanda hicho.
Amesema tayari baadhi ya makampuni yamekuwa yakiweka oda kwaajili ya kupata sukari inayozalishwa katika kiwanda hicho ambacho kimekuwa na manufaaa makubwa kwa wananchi na vijana kwa kupata ajira na kujiongezea kipato chao.
Ziara hiyo imefanyika lengo likiwa ni kukagua na kujiridhisha namna kiwanda kinavyofanya kazi ikiwemo mashamba ya miwa pamoja na mabwawa kwaajili ya umwagiliaji.