Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri ya Bumbuli Baraka zikatimu
Mwenyekiti wa Halmashauri Ya Bumbuli Amir Shehiza akimkabidhi Mwalimu jiko la gesi yaliyotolewa na Mbunge Wa Jimbo Hilo January Makamba.
……………………
Raisa Said,Bumbuli
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli imetangaza mikakati kadhaa yeye lengo la kuinua kiwango cha ufaulu na elimu kwa ujumla katika halmashauri hiyo.
Kwa muijibu wa Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Baraka Ziakatimu, Halmashauri imelenga kuongeza kiwango cha ufaulu wa mtihani wa upimaji kidato cha pili kutoka asilimia 84 hadi kufikia 100 na wa kidato cha nne kuongezeka kutoka asilimia 89.58 hadi kufikia 95.
Akizungumza katika kikao cha wadau wa elimu wa Halmshauri hiyo, aliitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja kutoa motisha ya fedha taslimu kwa wanafunzi, walimu na shule zitakazofanya vizuri.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa wamepanga kutoa motisha ya Sh million 3 kwa kila shule ya sekondari ambayo itakuwa na ufaulu wa divisheni 1 kwa wanafunzi wote (asilimia 100). Kuna jumla ya shule 29 za sekondari za kata katika Halmashauri hiyo.
Alieleza kuwa shule ambayp itakuwa na divisheni ya pili itapata Sh milioni 2 wakati shule ambayo itakuwa haina divisheni zero Wala four itapata Sh milioni moja.
Halmashauri hiyo mwaka huu imetoa jumla ya Sh milioni 3.63 kama motisha kwa walimu 134 waliowawezesha wanafunzi kupata ufaulu wa Daraja A na B katika mitihani ya upimaji wa kidato cha pili.
Pia Halmashuri imetoa motisha ya jumla ya Sh millioni 4.11 kwa walimu 118 waliowawezesha wanafunzi kupata ufaulu wa daraja A na B katika mitihani ya kidato cha nne. Pia imetoa motisha ya jumla ya Sh 300,000 kwa walimu watatu wa taaluma kutoka shule za serikali zilizofuta daraja sifuri katika mitihani ya kidato cha nne. Shule hizo ni Mgwashi, Kizanda na Kizimba.
Naye Afisa Elimu Taaluma (Sekondari), Simon Shelukindo, alitaja baadhi ya changamoto zinazokabili elimu kuwa ni pamoja na walimu kukaa kwenye vituo kwa muda mrefu hali inayowafanya kufanya kazi kwa mazoea. Alisema hali hiyo inasabishwa na ukomo wa bajeti ya Msawazo kwa walimu (Uhamisho) kuwa finyu.
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni wanafunzi wanaofeli kidato cha pili kutorejea shule wakati ambapo serikali imetoa nafasi ya a hawa kurudia shule pindi alama za ufaulu kutokidhi kuendelea na kidato cha tatu.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Amiri Shehiza alisema katika mwaka 2022/23 serikli inaoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan imetoa jumla ya Sh Bilioni 1.16 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu ikiwemo ujenzi wa nyumba nane za walimu katika shule nne ambazo hazikuwa na nyumba za walimu (Sh milioni 228 kutoka tozo ya mawasiliano.
Miradi mingine ni ujenzi wa shule ya sekondari ya Kwehangala kupitia mradi wa SEQUIP (Sh mlioni 584,) ukamilishaji wa maboma ya maabara za sayansi katika shule tatu (Sh milioni 150) na ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa katika shule saba (Sh milioni 200).