NA SOPHIA KINGIMALI.
Serikali ya Tanzania na Hungary wamesaini mkataba wa ushirikiano katika sekta ya maji kwa sababu nchi hiyo inaongoza duniani kwa kudhibiti mafuriko maji safi na maji taka hivyo kupata ujuzi wa teknolojia
Huku Pia nchi hiyo inatarajia kufanya uwekezaji wa Kiwanda cha kutengeneza ndege ndogo Mkoani Morogoro.
Akizungumza leo Machi 28 jijini Dar es Salaam baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amesema ugeni huo umekuja baada ya Rais wa Hungary kufanya ziara yake ya kikazi nchini mwaka 2023.
“Tumefanya mazungumzo ya kiserikali ikiwemo ushirikiano wa kibiashara kufanya makongamano ya kibiashara nchi hizi mbili kufanya ziara za kibiashara kwa sekta binafsi.
” Pia mazungumzo mengine ni kuhusu sekta ya utalii ambapo miaka miwili iliyopita watalii walikuwa 5000 hadi sasa watalii wamefika 11000 na hili ni ongezeko kubwa la watalii kutoka Hungary “amesema Makamba.
Amesema wanatajia kusaini mkataba wa usafiri wa anga kuwezesha ndege kusafiri moja kwa moja kutoka Hungary hadi Tanzania ambapo Makamba amewaahidi kuwapa rasimu ya mkataba huo ili waanze safari hizo mara moja.
Vilevile, wamezungumza namna ya kushirikiana katika elimu watanzania walio nufaika na ufadhili wa masomo 146 ambapo Nchi ya Hungary ilitoa ufadhili wa masomo 30 na Tanzania tano.
Ameongeza kuwa wanatarajia kufungua ubarozi nchini ili kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Peter Szijjàrtò amesema walikuwa na mazungumzo mazuri na nchi hizo mbili zina ushirikiano katika mambo mbalimbali.
“Tulikuwa na mazungumzo tumezungumzia sekta ya maji, elimu, utalii na kuhusu usafiri wa anga tutasaidia nchi ya Tanzania katika sekta hizo na kubadilishana ujuzi na uzoefu kati ya Hungary na Tanzania,”amesema Szijjàrtò