Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ameipongeza ACB kwa kuandaa hafla ya kufuturisha wateja, Wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Benki hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena tarehe 25 Machi, 2024, akiongea katika hafla hiyo ambayo Mhe.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi, Mhe. Mpogolo amesema kwamba “kitendo cha kufuturisha kilichofanywa na ACB ni ibada ambayo mwanadamu aliyetunukiwa zaidi anatoa kwa wengine na atapata thawabu kwa kufanya hivyo”.
Aidha, ameipongeza ACB kwa kuwa sehemu ya ukuwaji wa uchumi wa Tanzania na kuahidi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuwa karibu na taasisi za fedha hususan benki ya Akiba katika kuinua uchumi wa nchi na kuleta maendeleo katika jamii.