Machi 27, 2024, Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye pia anawakilisha Ufalme wa Eswatini na Jamhuri ya Madagascar, amekutana na Mhe. Jane Matty Mkhonta-Simelane, Waziri wa Utalii na Mazingira wa Ufalme wa Eswatini, Jijini Mbabane.
Mkutano huo ulifanyika wakati wa Ziara ya Kikazi ya Mhe. Balozi Kasike Ufalme wa Eswatini ambako anakutana na Viongozi wa Serikali na Taasisi mbalimbali zinazoshughulika na Masuala ya Uchumi, Biashara na Uwekezaji kwa ajili ya kutangaza fursa na kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania.
Pamoja na masuala mengine, Viongozi hao wawili walikubaliana kuanzisha na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Eswatini katika Sekta ya Utalii hasa kutokana na vivutio mbalimbali vilivyopo kwenye nchi hizi mbili.
Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania – Maputo