Na Sophia Kingimali.
Wizara ya Viwanda na Biashara imefanya mazungumzo na wawekezaji kutoka nchi ya China waliokuja kuangalia fursa zinazopatikana ili waweze kuwekeza nchini na nchi iweze kunufaika kwa kupata uwekezaji utakaochochea maendeleo ya nchi na kuongeza ajira.
Akizungumza leo Machi 27 jijini Dar es Salaam baada ya mazungumzo hayo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Sempeho Manongi amesema wamepata wageni kutoka nchini China katika Jimbo la Changzho ambao wamekuja kwaajili ya kuangalia maeneo ambayo wanaweza kuleta ushirikiano.
Amesema wawekezaji hao wameletwa kwa kushirikiana na kampuni mbili ambazo ni kampuni ya Canopus Energy Solutions na Amec Group katika wangeni hao wameambatana na viongozi wa serikali na wawekezaji na timu ya wataalam.
“Tumewaonyesha fursa zilizopo za viwanda na maeneo ya uwekezaji katika sekta zote muhimu kwa nchi yetu ili waweze kuimarisha uchumi wa nchi.Pia wamewaonyesha maeneo mengine ya viwanda ambayo ni muhimu wanaweza kuzalisha na kutengeneza Kituo maalumu,”amesema Manongi.
Ameeleza kuwa katika mazungumzo hayo wamekubaliana na baadhi ya maeneo hayo hivyo wanaelekea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),kwenda kupata taarifa ya kina kwenye masuala ya uwekezaji ili waweze kuingia makubaliano kwenye maeneo ambayo wameona yanahitajika kwaajili ya uwekezaji.
Manongi amesema wao wameonyesha maeneo ya sekta ya kilimo katika kuongeza thamani mazao ya kilimo maeneo ya uzalishaji wa madini ya viwanda ambayo ni muhimu mfano chuma
Ameongeza kuwa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) wana maeneo makubwa ambayo wanaweza kuwekeza ikiwemo Kilimanjaro machine tools, Tange lipo Tanga, Kibaha maeneo kwaajili ya uwekezaji.
Amesema wameshauriana kuangalia aina ya uwekezaji kwani wanaweza kuwekeza moja kwa moja, au kuwekeza kwa ubia na kubadilisha ujuzi na uzoefu ambao utaletwa nchini.
Aidha amesema katika Miradi saba ikitekelezwa kuzalisha MEGAWATI
zaidi ya 1400 wanahitaji umeme kwa wingi hivyo wakipata uwekezaji kikubwa kupata utalaamu wa hiyo sekta ndio wanahitaji kwa wingi na baadae wawekezaji wakijitokeza watapata umeme kwa wingi na uzalishaji utaongezeka ajira na matumizi ya umeme.
Naye Kiongozi wa Ujumbe Kutoka Serikalini ya Jimbo la Changzho, Shen Don amesema nchi hizo mbili zimekuwa na ushirikiano mkubwa katika nyanja mbalimbali wanahitaji kuwekeza katika uzalishaji katika viwanda.
Kwa upande wake Mhandisi Anna Nyangasi wa Kampuni ya Canopus Energy Solutions kwa kushirikiana na Amec amesema kampuni hizo zimewaleta wawekezaji hao ili kuja kuwekeza nchini kwenye meeneo tofauti ya kiwemo sekta ya kilimo,Afya na vifaa vya ujenzi
“Watawekeza katika maeneo mashine za kilimo watawekeza dola za kimarekani milioni 24.5, vifaa vya hospitali watawekeza dola za kimarekani milioni 6.
Vifaa vya umeme watawekeza dola za Kimarekani milioni mbili vifaa vya ujenzi dola za kimarekani milioni 11.3 vifaa vya uchakataji wa mafuta dola za kimarekani milioni 43,”amesema Mhandisi Anna .