Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam Edward Mpongolo akizungumza na wanahabari ofisi kwake akitoa tathmini ya mwenendo wa maendeleo ya wafanyabiashara wa soko la Kariakoo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo Martin Mbwana akiwaeleza wanahabari namna walivyojipanga kushirikiana na serikali katika shughuli zao.
Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Jomaary Mrisho akiwaeleza wahabari tathmini ya mwenendo wa maendeleo ya wafanyabiashara wa soko la Kariakoo.
……………….
NA MUSSA KHALID
Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam imewataka wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga kuendelea kuzingatia taratibu zilizowekwa za ufanyaji wa biashara zao ikiwemo kutorudi maendeo ambayo waliondoshwa awali.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo wakati akizungumza na wanahabari akitoa tathmini ya mwenendo wa maendeleo ya wafanyabiashara wa soko la Kariakoo.
Mpogolo amesema waliunda timu ya pamoja ya kuangalia changamoto ambazo zinawakabili,ambapo wamebaini kuna baadhi ya maeneo ambayo wafanyabiashara wamerejea licha ya kuzuiwa jambo linalosababisha ukwepaji wa kodi.
Aidha amesema kuwa maadhimio ambao wamekubaliana ni pamoja na kuimarisha usafi katika soko hilo ikiwa ni pamoja nakuwapa tahadahri wafanyabiashara wanaotoa mizigo nje.
‘Wafanyabiashara ndogondogo wamerudi sasa katiba baadhi ya maeneo ambayo hapo awali tuliyazuia na tukawapanga katika maeneo yao stahili hivyo wamerudi na wengine wanatumia miamvuli ambapo wanazuia huduma katika maduka mengine’amesema DC Mpogolo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Jomaary Mrisho amesema kuwa jambo hilo limewashirikisha wamachinga kwa ujumla ili kupata ufumbuzi baada ya kujadili kwa kina kuhusu hali ilivyo Kariakoo.
Amesema kuwa malengo ni kuwezesha soko hilo la kimataifa wafanyabiashara waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo Martin Mbwana amesema kamati iliyoundwa wamekubaliana kwa pamoja namna ya kufanya baishara katika soko hilo.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya amesema wameanza kuweka jitihada katika jiji la Dar es salaam ikiwemo kufunga taa katika mitaa mbalimbali katika soko hilo ili wafanyabiashara waweze kufanya biasharazao kwa masaa 24 kwa uhuru.