Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Zanzibar kupata bahati ya kua Mwenyeji wa Mashindano ya Challeng Senior Cup yatakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Sita mwaka huu hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Migombani Zanzibar.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya Waandishi wa Habari alipozungumza nao kuhusiana na Zanzibar kupata bahati ya kua Mwenyeji wa Mashindano ya Challeng Senior Cup yatakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa Sita mwaka huu hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Migombani Zanzibar.
……..
Na Rahma Khamis Maelezo 26/3/2024
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amewataka wananchi kutoa ushikiano katika maandalizi ya Mashindano ya Challenge senior Cup yanayotarajiwa kufanyika Zanzibar.
Wito huo ameutoa huko Ofisini kwake Migombani wakati akitoa taarifa kuhusiana na Zanzibar kuchaguliwa kuwa Mwenyeji wa Mashindano ya Challenge senior Cup yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka 2024.
Amesema mashindano hayo ambayo yalifanyika nchini Uganda mwaka 2019 yamerudi tena ambapo Zanzibar imebahatika kufanyika katika Uwanja wa News Amani Complex na yatashirikisha Nchi tofauti ikiwemo Kenya, Uganda Sudan na Somalia kulingana na utaratibu .
Aidha amemshukuru Dkt. Hussein Mwinyi kwa maono yake na kuweza kuufanyia ukarabati mkubwa uwanja huo ambao umepelekea kupewa uwenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Waziri Tabia amefahamishakuwa katika kuhakikisha Zanzibar inafanya vizuri katika michuano hiyo ameamua kuirejesha kamati ya Saidia Zanzibar Ishinde (SAZI) ambayo ilikuwepo kwa awamu mbalimbali huko nyuma.
“Lengo kuu la kamati hii ni kuisaidia Serikali katika kutafuta fedha za kuziendesha timu zetu za Taifa, lakini pia kuisaidia katika maandalizi bora ya mashindano haya’ alifafanua Waziri.
Akizungumzia kuhusu kamati hiyo Waziri Tabia ameeleza itaundwa Viongozi mbalimbali wakiwemo Mhe. Ayoubu Muhammed Mahmoud ambae ni Mjumbe, Ndg Said Kassim Marine (Katibu) Mhe. Nassor Ali Jazira na Mhe Ussi Salim Pondeza.
Wengine ni Mhe. Fatma Ramadhan Mandoba, Ndg. Arafat Ali Haji, Ndg. Mwalimu Ali Mwalimu,Ndg Naima Said Shaame,Ndg Ramadhan A. Bukini pamoja na Mhe. Abdulghafar Idrissa Juma.
Hata hivyo Waziri amewaomba wananchi kuwa wakarimu katika kipindi chote ambacho wageni watakuwepo hadi kumalizika kwa mashindano hayo ili kutimiza azma ya Zanzibar ni njema kwa Amani na utulivu uliopo.