WAKULIMA wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi wametakiwa kuendelea kujiunga na vyama vya ushirika kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao kwa kupata bei nzuri sokoni.
Akizungumza na mwandishi wa habari afisa ushirika Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Tunu Goagoa alisema kuwa wakulima wakijiunga na vyama vya ushirika wakulima wanapata faida kubwa sokoni kuliko kuuza mazao nje ya ushirika.
Goagoa alisema kuwa wakulima wa wilaya ya Nachingwea wanapata manufaa mengi kwa sababu wamejiunga na ushirika na wanafurahia kuendelea kilimo wakiwa wanauza mazao kutumia ushirika.
Aliwataka wakulima ambao hawajajiunga na vyama vya ushirika wakajiunge ili waweze kupata faida zilizopo kwenye ushirika, ushirika wilaya ya Nachingwea upo makini na kila mkulima anapata faida kutokana na mazao yake.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima walisema kuwa wamekuwa wanapata faida kubwa kwenye ushirika kwa kuuza mazao kwa bei nzuri pamoja na kupata pembejeo za kilimo kwa bei ya ruzuku au bure muda mwingine.