Polisi Kata wa Kata ya Igamba Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi John Namayala Machi 25, 2024 amewakumbusha wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwanda majukumu yao wawapo shuleni na thamani yao pindi wakiwa wanafunzi ili kutimiza malengo ya masomo na maisha yao ya baadae.
Mkaguzi Namalaya ameeleza kuwa “Mwanafunzi anaejua thamani yake, kwa kusoma kwa bidii na kujiepusha na makundi maovu ambayo yatamuingiza kufanya vitendo vya kihalifu ni lazima atafanikiwa katika masomo yake”
Mkaguzi Namayala aliongeza kwa kusema mnatakiwa kuwaheshimisha wazazi wenu kwa kufuata maadili yaliyomema na kuachana na mambo mabaya yatokanayo na utandawazi ili kubaki kwenye mila na desturi za nchi yetu kwa faida ya kizazi kijacho.
Baada ya kuyasema hayo Mkaguzi Namayala aliwashukuru wanafunzi hao kwa kuwa wasikivu na kuonesha ushirikiano kwa kusikiliza na kuuliza maswali ambayo yalionesha wamelewa alichowafundisha