Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakiangalia vifaa vya matibabu katika Jengo la Dharula la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua jengo hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakionyeshwa mojawapo ya mtambo wa kutengeneza chaki wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza Chaki na Vifungashio cha Ng’ami kilichopo Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa katika chumba cha kuhifadhi mitungi ya oksijeni katika Jengo la Dharula la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua jengo hilo.
………
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC),imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa utekelezaji mzuri wa mradi wa ujenzi wa Jengo la Dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.
Alisema Kamati inaipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa ujenzi mzuri wa Jengo la Dharula na kwa gharama halisi ambalo linawawezesha Watanzania kupata huduma inayostahili.
“Jengo ni zuri na vilevile kuna vifaa vya kisasa vinavyotoa huduma, katika mradi huu tunaona nia ya Mheshimiwa Rais ya kupeleka huduma kwa Watanzania kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya juu imetimia,” alisema
Alisema Kamati inaelekeza jengo hilo litunzwe na litumike kwa matumizi yaliyokusudiwa na kwamba liwe lifanyiwa ukarabati wa mara kwa mara ili lidumu kwa muda mrefu.
Kamati ya LAAC pia ilitembelea na kukagua Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza Chaki na Vifungashio cha Ng’ami katika Halmashauri hiyo ya Maswa na kuipongeza Halmashauri hiyo kwa kubuni mradi huo wa kimkakati.
“Huu ni mradi wa kimkakati na wa kipekee ambao Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imetumia fursa ya ‘material’ yanayopatikana hapa kuanzisha mradi huu, Kamati inatoa wito kwa Halmashauri nyingine kupitia mradi wa Maswa kuwa wabunifu kwa kuanziasha miradi ya kimakakati ambayo itakuwa na tija na itatengeneza ajira kwa Watanzania,” alisema.
Mheshimiwa Mabula alisema Kamati inaelekeza ujenzi wa Kiwanda hicho ukamilike ndani ya muda uliopangwa ambao ni Mei 15, mwaka huu.
Aidha, alitaka Halmashauri ya Maswa kuangalia namna ya kutafuta mapato ambayo yatawezesha kuwa na mashine ya vifungashio na kuona namna ambavyo kiwanda hicho kitajiendesha kibiashara.