Machi 25, 2024, Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji amekutana na Mhe. Dkt. Lidia Cordoso, Waziri wa Bahari, Mito na Uvuvi wa Jamhuri ya Msumbiji kwenye Ofisi za Wizara hiyo Jijini Maputo.
Kupitia mkutano huo, Viongozi hao walizungumza masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji katika Eneo la Uchumi wa Buluu hususan Uvuvi na Kilimo cha Mazao ya Bahari.
Ili kuwezesha ushirikiano wenye tija na maslahi kwa pande zote mbili, Viongozi hao walikubaliana kuanza mchakato wa Kusainiwa Hati ya Makubaliano (MoU) kuhusu Ushirikiano kwenye Eneo la Uchumi wa Buluu.
Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania – Maputo