Bw. Benjamini Charles Chuma mkazi wa Kilungule wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam amefunguliwa kesi ya jinai na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni yenye Namba (Cc.6600) kwa makosa ya kuomba na kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a) na 15(2), cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [CAP 329 RE 2019]
Mshtakiwa akiwa ni kiongozi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilungule Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imedaiwa mahakamani hapo kuwa aliomba Rushwa kiasi cha shilingi 120,000 na kupokea kiasi cha shilingi 100,000 ili asimchukulie hatua za kisheria Bw. Yuredi Mteseli Rwebugisa.
Mshtakiwa alisomewa mashtaka yake mbele ya Mheshimiwa Hakimu Erick Rwehumbiza ambapo alikana makosa yote.
Shauri hilo limepangwa kusikilizwa tena tena tarehe 28/03/2024.