Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akisisitiza jambo wakati akitatua mgogoro wa kudai fidia kutoka kwa familia Mwinyimanga wakati wa kutafuta suluhu ya mgogoro huo wilayani Kilwa mkoa wa Lindi tarehe 23 Mchi 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda akizungumza na familia ya Mwinyimanga yenye mgogoro wa fidia kwenye eneo la Pwani Masoko wilayani Kilwa. Mhe, Pinda alisikiliza na kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo tarehe 23 Mchi 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda pamoja na familia ya Mwinyimanga yenye mgogoro wa fidia katika eneo la Pwani Masoko wilayani Kilwa wakifuahi mara baada ya kupata ufumbuzi wa mgogoro huo tarehe 23 Mchi 2024.
Juma Faki Mjaka akimuonesha Naibu Wzairi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda eneo analodai kulimiki na kutwaliwa katika sehemu inapojengwa Bandari ya Kilwa mkoa wa Lindi tarehe 23 Machi 2024
……………………
Na Munir Shemweta, KILWA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleio ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda ameingilia kati mgogoro wa wananchi kwenye halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi wanaodai maeneo yao kutwaliwa bila ya kulipwa fidia.
Hatua hiyo ya Mhe, Pinda inafuatia kupewa malalamiko na Juma Faki Mjaka mkazi wa Kilwa anayedai kutwaliwa eneo lake inapojengwa Bandari ya Kilwa pamoja na familia ya Mwinyimanga inayodai kunyanyaswa kudhulimiwa eneo lao Masoko Pwani wilayani Kilwa.
Naibu Waziri alitembelea eneo inapojengwa Bandari ya Kilwa tarehe 23 Machi 2024 kwa lengo la kujiridhisha madai ya Mjaka na baadaye kukutana na familia ya Mwinyimanga wakati alipokwenda kufungua mkutano wa wadau kuhusu uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi katika wilaya ya Kilwa.
Baada ya kutembelea eneo inapojengwa Bandari ya Kilwa na kupata maelezo ya mlalamikaji Bw. Mjaka Mhe, Pinda aliagiza kuudwa Tume maalum itakayohusisha vyombo mbalimbali ili kubaini ukweli wa malamiko ya mwananchi.
Kwa upande wa familia ya Mwinyimanga inayodai kunyanyaswa na kutwaliwa ardhi yao kwenye eneo la Pwani Masoko katika halmashauri ya Kilwa, Naibu Waziri alitaka makubaliano yanayofikiwa baina ya wanaomiliki ardhi na wale wanaotaka kutwaa eneo kuzingatiwa.
Amesema, lengo la wizara yake ni kuondoa migogoro ya ardhi isiyo na sababu ya msingi hivyo asingependa kuona wananchi wakiendelea kulalamika kwa kudhulumiwa maeneo yao. ‘’Ulimkuta mtu umepapenda eneo lake fanya makubaliano, kimsingi mkishakubaliana tekeleza mlichokubalina’’ alisema Mhe. Pinda
‘’Ninachokuelekeza Mkuu wa wilaya fuata hayo hilo ambalo wamekataa kwa dhamira, ardhi ithaminiwawe na muekezaji afahamu kuwa eneo hilo lilikuwa na watu na mkuu wa wilaya hilo lizingatiwe’’ alisema Mhe, Pinda.
Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Pinda ameziagiza halmasauri zote nchini kujitayaarisha kabla ya kutwaa maeneo ya wananchi ili ziweze kulipa fidia kwa wananchi na kuondoa malalamiko.
Kwa mujibu wa Mhe, Pinda baadhi ya halmashauri zimekuwa tabia ya kutwaa maeneo ya wananchi bila kulipa fidia jambo linalosababisha kuwepo migogoro na malalmiko kutoka kwa wananchi.
‘’Halmashauri zijitayarishe kabla ya kutwaa maeneo maana nyingine hata baada ya kutwaa manep na kuyaendeleza zinashindwa kulipa fidia na hili linaleta sana malalamiklo kutoka kwa wananchi’’ alisema Mhe, Pinda.