Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (MNEC) ambaye pia ni mchumi,Richard Kasesela amewataka wa wananchi wa wilaya ya Kyela,Rungwe na Busokelo kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo ili kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Akizungumza na mwandishi wetu, Kasesela alisema kuwa wananchi wa wilaya hizo wanatakiwa kutumia vizuri fursa ya uwepo wa mazao ya Ndizi,Cocoa,Chai pamoja na uvuvi katika ziwa Nyasa kwa lengo la kukuza uchumi wao
Kasesela alisema kuwa wananchi wanatakiwa kulilinda na kulitunza ziwa la Nyasa ambalo limekuwa kivutio cha wageni na kuanza kufuga samaki kisasa ndani ya ziwa hilo hivyo wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo.
Alisema kuwa kwa sasa soko la samaki lipo juu, Cocoa na chai mazao hayo sokoni yana bei kubwa hivyo wananchi wanapaswa kuwekeza kwenye mazao hayo tofauti na zao la ndizi ambalo bado linamnyonya mkulima.
Kasesela alisema kuwa zao la ndizi shambani madalali hununua kwa shilingi elfu 2000 lakini hao huuza zaidi ya shilingi elfu 12000 jambo ambalo linawanufaisha madalali tofauti na wakulima.