*BRIQUETTES YA STAMICO SULUHISHO LA UCHUMI NA NISHATI MBADALA KWA WANAWAKE. NA SAMIA TAIFA
Machi 23/03/2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse ameshiriki katika Kongamano la Wanawake na Samia lililojumuisha wanawake kutoka mikoa 15 ya Tanzania, Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe Rosemary Senyamule.
Kupitia kongamalo hilo Vikundi vya wanawake na Samia wametoa shukrani zao za dhati kwa ushirikiano wanaoupata kutoka STAMICO.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake na Samia wa Mkoa wa Dodoma kwa niaba ya vikundi vingine amemshukuru STAMICO kwa kuendelea kuwasadia kumkomboa Mwanamke.
Kupitia mkutano huu wamemuomba Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO kukubali ombi la kuwa mjomba na mlezi wa karibu wa vikundi vya wanawake na Samia.
Aidha wanawake hawa wameshukuru jinsi STAMICO lilivyoweza kuonesha uthubutu kwa kuwapa uwakala wa Nishati Mbadala ya Rafiki Briquettes.
Akiongea katika jukwaa hilo Dkt Venance Mwasse alianza kwa kukubali ombi kutoka kwa Mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Dodoma la kuwa mjomba na mlezi wa wanawake na Samia nchini.
Shirika Mpaka sasa limeshawapa uwakala wa kuuza Mkaa wa Rafiki Briquttes kwa vikundi viwilli vya Wanawake na Samia vya Mikoa ya Geita na Dodoma. Na vikundi vingine 3 vimewezeshwa kwenye program ya upandaji miti. Vikundi hivi ni Wanawake na Samia wa Geita, Tanga na Zanzibar.
Kwa upande wa Mgeni rasmi Mhe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.Rosemary Senyamule amenza kuwashukuru wadau wote waliowezesha kongamano hilo kufanyika. Pia amemshukuru Dr. Venance Mwasse kwa kukubali kuwa mjomba na mlezi wa wanawake na Samia nchi nzima.
Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi wa mbalimbali pamoja na Mhe Anna Makinda, waheshimiwa wakuu wa wilaya za Dodoma, wakurugenzi na viongozi mbalimbali za Serikali pamoja na wadau wa Nishati safii za kupikia.
Sambamba tukio hilo STAMICO wameendelea kutoa elimu ya Nishati Mbadala wa Rafiki Briqutttes kupitia Kongamano