Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), Mheshimiwa Stanslaus Mabula akizungumza wakati Kamati ya LAAC ilipomtembelea Mkuu wa Mkoa Ofisini kwake katika Manispaa ya Musoma, kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Said Mtanda na kushoto ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mheshimiwa Patrick Gumbo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), Mheshimiwa Stansalus Mabula akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wakati Kamati hiyo ilipotembelea na mradi wa ujenzi wa Zahati ya Rwamlimi katika Manispaa hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakikagua mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Kata ya Kigera katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo.
………………….
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma kukamilisha ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Kata ya Kigera katika Manispaa hiyo katika muda uliopangwa.
Kamati ya LAAC ipo Musoma Mkoani Mara na leo imekagua mradi huo pamoja na mradi wa ujenzi wa Zahati ya Rwamlimi katika Manispaa hiyo.
Akitoa agizo hilo kwa niaba ya Kamati, Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalaus Mabula alisema pamoja na kutakiwa kumaliza mradi huo kwa wakati lakini pia gharama za ujenzi ziwe na uhalisia wa thamani ya mradi.
“Halmashauri mmeongeza kiasi cha shilingi milioni 153, mjitahidi mnapotekelelza mradi mhakikishe gharama hizo za nyongeza zinaendana na uhalisia,” alisema.
Kwa upande wa mradi wa Zahanati ya Rwamlimi, Mheshimiwa Mabula alisema Kamati inaagiza kiti kwa ajili ya chumba cha matibabu ya meno kifungwe haraka ili huduma hiyo iweze kuendelea.
Alisema pia Kamati inashauri Halmashauri hiyo kutumia fedha za mapato ya ndani kujenga njia za watembea kwa miguu katika Zahanati hiyo ili iwe na hadhi inayotashili.
Aidha, Kamati ilishauri kufanyika marekebisho mbalimbali katika majengo ya miradi yote miwili.