Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imeadhimisha Mafanikio ya Miaka 3 ya Mhe. Rais katika Mapambano dhidi ya Tatizo la Dawa za Kulevya katika Stendi Kuu ya Mkoa wa Arusha.
Miongoni mwa Mafanikio ya Miaka 3 ya Mhe. Rais Mkoani Arusha ni Royal Tour. Hivyo, DCEA Kanda ya Kaskazini ilichambua kwa kina “Mafanikio ya Royal Tour katika Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya nchini”.
Kwa mwaka 2023 DCEA ilifanikiwa kukamata zaidi ya Kilo 1,965,340.52 za dawa za kulevya. Pia ilifanikiwa kukamata kiwango kikubwa cha tani 3 ya dawa za kulevya kwa mkupuo katika historia. kwa Kanda ya Kaskazini zaidi ya gunia 237 na Kilo 310 za mbegu za bangi zilipata kuteketezwa wilayani Arumeru.
Katika Mafanikio ya Mhe. Rais katika Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya ni Kuanzishwa kwa Ofisi 5 za Kanda ikiwepo DCEA Kanda ya Kaskazini. Pia katika mafanikio ni kuimarishwa kwa huduma za matibabu, zaidi ya vituo 72 ziliboreshwa (16 MAT Clinic na 56 Sober House).
Viongozi mbalimbali walishiriki mdahalo huo wa wazi; ikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mkurugenzi wa Jiji, Afisa Elimu Mkoa wa Arusha, Mganga Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha, Kiongozi wa Daladala, Kiongozi wa Bodaboda, Pia wananchi wa stendi walihudhuria kuchangia mada mbalimbali zilizowasilishwa.