Katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji katika sekta ya Elimu, tarehe 22 Machi 2024, Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji alikutana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Joaquim Chissano, Prof. José Magode kwenye Ofisi za Chuo hicho zilizopo Jijini Maputo.
Katika Mkutano huo, pamoja na masuala mengine ya ushirikiano, Viongozi hao wawili walikubaliana kuanzishwa Darasa la Lugha ya Kiswahili Chuoni hapo ambapo Ubalozi uliahidi kusaidia kupatikana kwa Walimu watakaofundisha Darasa hilo.
Imetolewa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Maputo.
22 Machi, 2024