Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa Usafiri wa Anga na Msimamizi wa Kituo Kituo Cha Hali ya Hewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Bw. John Mayunga (wa kwanza kushoto) akitoa elimu kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati walipotembelea Kituo hicho leo Machi 23, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Kituo Cha Uangazi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Ally Selemani akifafanua jambo kuhusu utendaji wa Kituo hicho.
Afisa Mwandamizi Kituo Cha Uangazi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwaelimisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bariadi namna wanavyotabiri taarifa za hali ya hewa.
Afisa Mhangazi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitoa ufafanuzi namna wanavyotabiri taarifa za hali ya hewa za anga (Upper Air).
Afisa Mhangazi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Bi. Pamela Gabriel akiwaelimisha Wanafunzi kuhusu vifaa mbalimbali vinavyotumia kukusanya taarifa za hali ya hewa.
Afisa Mwandamizi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Bi. Pamela Gabriel akitoa ufafanuzi.
……..
Kituo Kituo Cha Hali ya Hewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) imeadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani kwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wa maendeleo, huku wakiitaka jamii kufatilia taarifa za hali ya hewa ili kuepukana madhara yanayoweza kujitokeza kutokana mabadiliko ya hali ya hewa na Tabianch
Akizungumza leo Machi 23, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akitoa elimu kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) na Shule ya Msingi Bariadi walipotembelea Kituo Kituo Cha Hali ya Hewa JNIA, Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa Usafiri wa Anga na Msimamizi wa Kituo Kituo Cha Hali ya Hewa JNIA, Mamala ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Bw. John Mayunga amesisitiza umuhimu wa jamii kufatilia taarifa za haki ya Hewa.
Bw. Mayunga amesema kuwa serikali imewekeza nguvu kubwa katika miundombinu ya hali ya hewa ikiwemo kununua vifaa ikiwemo rada pamoja na vifaa vingine vya kupimia hali ya hewa ili kuleta ufanisi wenye tija kwa Taifa.
“Mamlaka ya Hali ya Hewa ina wataalamu wengi waliosoma ndani na nje ya nchi ambao wanafanya kazi kwa uweledi kwa ajili kuisaidia jamii kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo ” amesema Bw. Mayunga.
Amesema kuwa TMA inakitengo ambacho kinahusika katika usafiri wa anga kwa kutoa huduma kwa ajili ya kuhakikisha usafi wa anga unakuwa Salaam muda wote.
Bw. Mayunga amesema kuwa wanaendelea kutoa huduma za taarifa za hali ya hewa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kabla ya ndege kuruka, ikiwa angani na wakati wa kutua.
Amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa uweledi katika kuhakikisha waatoa taarifa kwa usahihi.
Ameeleza kuwa mwaka huu kumekuwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo mvua kubwa ambapo maeneo mengi yamepata mafuriko pamoja na ongezeko la joto la juu, hivyo ni muhimu kuwa na utamaduni wa kufatilia taarifa hizo.
“Sisi tunaendelea kutoa tahadhari kwa wakati na siku ya leo tunaadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani kwa kutoa elimu kwa jamii na kujua namna tunavyofanya kazi” amesema Bw. Mayunga.
Nao baadhi ya wanafunzi Peter Mazuri kutoka Chuo Kikuu UDSM pamoja na Merry Kigoda wa Shule ya Msingi Bariadi wameishukuru TMA kwa kuwaelimisha kuhusu utendaji wa kazi zao jambo ambalo ni rafiki katika kuhakikisha wanakuwa na uwelewa katika matumizi ya taarifa ya hali ya hewa pamoja na kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
Maadhimisho ya Hali ya Hewa Duniani 2024 yamebeba kauli mbiu isemayo “Kuwa mstari wa mbele kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi”