Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amelipongeza Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kazi nzuri ya kuimarisha ulinzi na usalama.
Mhe. Serukamba ametoa pongezi hizo Machi 22, 2024 kwenye kikao na Maafisa, wakaguzi na askari wa Jeshi la Polisi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ofisini kwake ikiwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali kuhusu kazi za polisi.
“Nawapenda sana Polisi, mnafanya kazi iliyotukuka mnastahili pongezi, endeleeni kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ili kujenga imani kwa wananchi mnaowahudumia” – Mhe. Serukamba.
Naye kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani iringa, Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Allan Bukumbi amemshukuru mkuu wa mkoa kwa pongezi hizo na kuwataka askari kutenda haki na kutoa huduma bora kwa jamii ili kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya jeshi la polisi na wananchi.