Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Adinani Mpyagila amekabidhi Meza na viti 258 vyenye zaidi ya thamani ya shilingi milioni 19 kwaajili ya kidato cha kwanza 2024 katika shule 5 za sekondari wilaya humo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi samani hizo Mpyagila alisema kuwa wamemaliza tatizo la madawati katika wilaya hiyo baada ya kupokea maombi ya shule zote za sekondari ambazo zilikuwa na uhaba wa madawati.
Mpyagila ametoa agizo kwa afisa elimu sekondari kuhakikisha shule zote zinafanya ukarabati wa viti na meza kupitia fedha wanazopata kwaajili ya uendeshaji wa shule.
Mpyagila amewataka wanafunzi kutunza madawati hayo na kuwataka walimu kuwa wakali kwa mwanafunzi yoyote atakaye haribu madawati hayo huku akiwaagiza walimu kuongeza ufaulu wa masomo.
Kwaupande wake kaimu afisa elimu sekondari Samweli Honza ameishukuru Halmashauri kwa kutenga fadha za kutengeneza madawati hayo kwaajili ya kidato cha kwanza 2024 huku akisema kuwa madawati hayo pamoja na viti ni kwaajili ya shule za Nambambo,Rugwa Boys,Namatula na Mkotokuyana sekondari.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa shule hizo msimamizi wa mradi uwo mwalimu mkuu shule ya sekondari Nambambo Johari Mussa amesema kuwa madawati hayo yanakwenda kuwa suluhusho la kukabiliana na wazazi ifikapo 2024.