Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Meneja Mauzo wa Kampuni ya Gasi ya Orxy , Shaban Fundi (wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Zone no.7 wa Soko la Samaki la Kimataifa Feri Jijini Dar es Salaam, Saidi Mpinji wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kulia).
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gesi ya Orxy, Benoite Araman wakiwasikiliza wafanyabiashara wa samaki katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mmoja wa mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.
…………………..
Na Sophia Kingimali
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Abbas Mtemvu amewataka mama Lishe na baba lishe kuendelea kutumia nishati safi ya kupikia na kuchangamkia fursa zinazojitokeza pindi ujenzi wa barabara zaidi ya kilometa 200 utakapoanza kwa kupeleka chakula pindi ujenzi unapokuwa unaendelea.
Hayo ameyasema leo March 22,2024 katika soko la samaki la kimataifa Feri Jijini Dar es salaam wakati wa kugawa mitungi 200 kati ya 700 iliyotolewa na kampuni ya gesi ya ORYX Tanzania kwa kushirikiaba na Mbunge wa ilala kwa Mama/baba lishe waliopo sokoni hapo.
Amesema serikali imeendelea kupeleka maendeleo kwa wananchi lakini pia kuhakikisha adhima ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inatimia ya kuhakikisha kila mwananchi anatumia nishati safi ya kupikia ili kuendelea kutunza mazingira.
Aidha Mtevu amewataka mama na baba lishe hao kujiandaa katika vikundi ili waweze kupata mkopo kutoka kwa serikali kwani kiasi cha bilioni 8 kimetengwa kwa ajili ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwani muda si mrefu itaanza baada ya kusimama mwa muda.
“Serikali ipo tayari kukupeni mitaji na imejipanga vizuri sasa jiandaeni kuchangamkia fursa kwani Aprili mwaka huu utaanza ujenzi mkubwa wa barabara zaidi ya km 200 ambapo zaidi ya bilioni 188 zitatumika sasa hii ni fursa kwa baba na mama lishe kuhakikisha mnapeleka chakula cheni ili kujiongezea kipato”,Amesema.
Kwa upande Naibu spika na Mbunge wa Ilala Musa zungu amesema wanatarajia kufunga mtambo wa kisasa wa nishati safi ya kupikia katika soko hili ili kuwasaidia wafanyabiashara kununua gesi hiyo kutokona na matumizi yao yaani kama mfumo wa luku.
Amesema tayari wameshafanya mazungumzo na kampuni ya ORYX TANZANIA na tayari wamekubali kufunga mfumo huo wa kisasa kisha kusambaza huduma kwa wafanyabiashara kwa gharama nafuu.
“Mkombozi wetu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye alianziasha kampeni ya nishati safi ya kupikia ili kuhakikisha watanzania wanaishi maisha mazuri lakini pia mazingira yanatunza”,Amesema.
Naye Mkurugenzi mkuu wa ORYX Tanzania Benoit Araman amesema wanaendelea kutekeleza mkakati wa Rais Dkt Samia wa kuhakikisha matumizi ya nishati safi ya kupikia yanafikiwa na kila mwananchi ili kulinda mazingira na afya za watumiaji.
Amesema walianza mkakati wa kusaidia matumizi ya nishati safi tangu Julai 2021 baada ya serikali kutangaza inataka hadi kufikia 2030 asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia ambapo wameahaidi kushirikiana na serikali ili kuhakikisha adhma hiyo inafikiwa.