WANAWAKE wapenda maendeleo wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi wametoa msaada wa shilingi millioni 45 kwa wahanga wa mnyama Tembo na wafugaji ambao wamesababisha madhara makubwa kwa jamii.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo wanawake hao walisema kuwa wameamua kujitolea kutokana na kuona madhara ambayo wananchi wa kata ya Ngunichile na Nditi wameyapata kutokana na mnyama Tembo na wafugaji.
Walisema kuwa msaada huo umetokana na harambee waliyoifanya swali ambayo kwa asilimia kubwa ndio imesaidia kupatikana kwa msaada huo.
wamefanya harambee kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa Tembo na wafugaji katika kata ya Nditi na Ngunichile
Walisema kuwa wanashukuru idara ya maendeleo ya jamii ya Nachingwea kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kufanikisha kupatikana kwa msaada huo.