Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kupaa kwa kusaini Mkataba mwingine mnono wa uchorogaji na Mgodi wa Buckreef uliopo Mkoani Geita. Mkataba huo umesainiwa tarehe 20 Machi 2024 mbele ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe Martin Shigella.
Mkataba huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi Billioni Tano ni kwa ajii ya kufanya utafiti zaidi wa madini ili kuongeza thamani na maisha ya Mgodi wa BuckReef.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa Mkurugezi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse ameushukuru Mgodi wa BuckReef kwa kuamini kufanya kazi ya Uchorogaji na STAMICO.
Dkt Mwasse katika hotuba yake alieleza jinsi Shirika linavyofanya mageuzi makubwa ya kujiendesha kibiashara kuunga mkono “R4” za Mhe Rais. “STAMICO tumejikita kwenye R mbili ambazo ni Reform na Rebuild tunashukuru na tunaahidi kuendelea kuyaishi mageuzi haya ya Mhe Rais” alisema Dkt Mwasse.
STAMICO ina miradi mikubwa ya Uchorogaji kwenye Migodi ya GGM, Shanta Gold na BuckReef
na Vituo viwilli vya mfano kwa ajili ya wachimbaji wadogo vya Lwamgasa na Katente.
Aidha STAMICO imewawezesha Wanawake na Samia wa Mkoa wa Geita kwa kuwapa uwakala wa kuuza Nishati Mbadala ya Rafiki Briquettes ili waweze kujipatia kipato. Kikundi hiki kimeshakabidhiwa container la kuuzia Nishati hii kwa sasa wanaendelea na maboresho ili waweze kuanza kuuza Nishati hii mwezi Aprili 2024.