Vijana wametakiwa kutumia bunifu mbalimbali, kuendana na soko la ajira, kubadilisha mtazamo uliopo, kusubiri ajira kutoka Serikalini.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judith Nguli wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, walioshiriki Siku ya Mzumbe na Kambi ya Wajasiliamari inayofanyika Kampas Kuu Morogoro.
Katika siku ya pili ya Mzumbe na Kambi ya wajasiliamari Chuo Kikuu Mzumbe, wanafunzi wamepata muda kuwasilisha na kushindanisha mawazo ya biashara na mshindi wa Kwanza amepata shilingi milioni moja ya kitanzania, Mshindi wa pili shilingi Lakin Saba na watatu laki tatu.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwigoha amesema kupitia Mradi wa HEET Mzumbe imepata Dora za kimarekani million 21, hivyo kupitia mradi huo Chuo Kikuu Mzumbe itakuwa kituo ( center) ya wajasiliamari.
Amesema kwa mwaka huu wa 2024 Chuo kimeongeza wanufaika zaidi ya 20 kutoka nje ya Chuo ambao wananufaika na Kambi ya wajasiliamari, wakikenga kujenga mahusiano mazuri na wadau pamoja na kutoa fursa kwa wanafunzi kupata uzoefu kutoka kwa makampuni makubwa.
“Kila mwaka vijana lakin 8 wanaongezeka kwenye soko la ajira hivyo serikali haiwezi kuajiri watu wote hivyo Chuo Kikuu Mzumbe kimekuja na Mwarobaini wa kutatua changamoto ya ajira”. Amesema Prof. Mwegoha
“Mzumbe tumeamua kuingia kwenye hii safari kuwa na wahitimu wenye ushindaji kwenye solo la ajira,pia wanaoweza kujiajiri watokapo hapa”. Amesema makamu Mkuu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Mwegoha