Na Joel Maduka ,Msalala,Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Shinyanga Mabala Mlolwa ameitaka halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Kuhakikikisha inarejesha kiasi cha Sh,Milioni16 wanazirejesha kwa wanufaika wa mfuko wa TASAF kwenye Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Mabala Mlolwa ameoneshwa kuchukizwa na kitendo kilichofanywa na watumishi wa Halmashauri hiyo kwa kutafuna fedha za wanufaika wa mfuko wa maendelo ya jamii TASAF jambo ambalo ni kinyume cha Sheria.
Mabala amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhakikisha fedha hizo zinapatikana na kufikia ijumaa ziwe zimerudishwa.
“Kusimamishwa watumishi sio kigezo tunachotaka ni pesa irudishwe yani kweli unakula pesa ya mtu masikini uoni hata aibu kabisa harafu Kaimu Mkurugenzi unakuja unatuambia eti umewasimamisha watumishi hii kauli sikubaliani nayo Mpigie simu Mkurugenzi mtendaji wa Msalala Mwambie Mwenyekiti anataka pesa ya wanufaika wa TASAF ilipwe sikubali kuona uonevu wa kwa wananchi”Mabala Mlolwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga.
Kufuatia maelekezo hayo Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Mfilinge Abdullah amesema wanaendelea na juhudi ya kuhakikisha fedha hizo wanazirudisha kwa wananchi na tayari watumishi ambao wameonekana kwenda kinyume na fedha hizo wameshasimamishwa kazi.
“Mhe Mwenyekiti nikuhakikishie kiasi cha Milioni 16 ambazo zimebakia tutahakikisha tunazirudisha kwa wakati kwa wanufaika wa mfuko wa TASAF tunaomba mtusamehe tu kwani tayari tunaendelea na mchakato wa Malipo ya Fedha zote zinazodaiwa”Mfilinge Abdulllah Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala,Mibako Mabubu amemuhakikishia Mwenyekiti wa CCM Kuhakikisha ifikapo Ijumaa ya wiki hii pesa zote zitakuwa zimefika kwa walengwa.Huku Mbunge wa Msalala Iddi kassim Iddi akihaidi kushughulika na watu ambao wataonekana kudhurumu haki za wananchi.