Na Joel Maduka Geita
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa MNEC Chacha Wambura (WAJA),amesema mikakati ya chama cha mapinduzi ni kuona jumuiya zake zinakuwa na uchumi imara na zinaweza kujiendesha zenyewe bila ya kutegemea fedha kutoka makao makuu ya chama.
MNEC Waja amesema hayo wakati akikabidhi usafiri wa Baiskeli zipatazo 34 kwa jumuiya ya vijana (UVCCM)na wanawake (UWT) pamoja na majoro 10 ya kushonea sare za chama kwenye jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM Wilaya ya Geita.
Amesema nia ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano ni kuona chama hicho kinajengeka kwa kubuni miradi ambayo itaanzia ngazi ya shina,Kata ,Wilaya pamoja na Mkoa na kwamba wao kama viongozi wamekuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kwa kuona miradi ya chama inasimama na inakuwa na tija kwa wanachama.
“Sisi mikakati yetu kama Mkoa wa geita tunaendelea kutekeleza miradi ya kimikakati kwa kujenga ofisi kuu ya Mkoa na kujenga ukumbi wa kisasa ,Lakini pia kwenye Wilaya pia tumeendelea kujenga maduka ya kisasa nia yetu na malengo yetu tunaitaji kuona chama tawala kinakuwa na nguvu ya miradi mikubwa”Chacha Wambura MNEC
Aidha amesema ameamua kuongeza Baiskeli na kutoa kwenye jumuiya wa vijana na wanawake kutokana na mwanzoni alitoa kwenye jumuiya ya wazazi kwa lengo ni kuona jumuiya zote zinapata usafiri huo ambao utasaidia kuwafikia watu wengi zaidi katika kukiimalisha chama.
“Tumetoa Baiskeli tatu kwa kila kata zilizopo Halmashauri ya Mji wa Geita nia yetu kubwa ni kuona zinakwenda kukisaidia chama cha mapinduzi kupata wanachama wengi zaidi ,Lakini pia niliona namna vijana wa itifaki walivyokuwa wakipata shida ya kuwa na sare zisizo bora nimeguswa nimeamua kuwapatia majoro 10 kwaajili ya kushona sare zuri tunataka kuwaona vijana wa Wilaya yetu ya geita wanakuwa watanashati”Chacha Wambura.
Sanjali na hayo Waja amewataka wanaccm kujitokeza kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao unatarajia kufanyika Mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha chama hicho kinapata nafasi za kuongoza ngazi ya vijiji,mitaa na vitongoji.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Geita Naomi Fujo amemshukuru MNEC Waja kwa kuwa na moyo wa kujitolea kuzisaidia jumuiya zilizopo Wilayani Geita.