Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (Kulia) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen (katikati) kwa niaba ya Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, wakitia saini hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Thomas Terstegen. Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (Kulia) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen (katikati) kwa niaba ya Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, wakibadilishana Hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria, katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Thomas Terstegen.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (Kulia) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen (katikati) kwa niaba ya Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, wakionesha Hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria, katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Thomas Terstegen. Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (Kulia) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, akizungumza baada ya hafla ya utiaji saini Hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen.
Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen (katikati), akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta za maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya na Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Thomas Terstegen. Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (wa tatu Kushoto), Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Thomas Terstegen (watatu kulia) na Mkuu wa Idara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani, Bw. Marcus Von Essen ( wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania na Ujumbe kutoka Shirikisho la Ujerumani, baada ya hafla ya Utiaji saini wa hati za Makubaliano ya ahadi (commitment) ya msaada wa kiasi cha Euro milioni 70 (sawa na shilingi bilioni 193.71) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania, ikiwemo Sekta ya maji, Afya, Maliasili, Utawala Bora na Usimamizi wa Sheria. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam.
……………………….
Na Sophia Kingimali, Dar es Salaam.
Serikali ya Tanzania na serikali ya Ujerumani zimesaini makubaliano ya ahadi ya msaada wa kiasi cha bilioni 193.71 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya maji,Afya,maliasili,utawala bora na usimamizi wa sheria.
Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo leo March 20,2024, jijini Dar es salaam Naibu Katibu mkuu wizara ya Fedha Elijah Mwandubya amesema fedha hizo zitasaidia kuziunganisha sekta za maendeleo nchini katika eneo la Bioanuai.
Amesema eneo la Bioanuai linajumuisha kusaidia hifadhi za taifa hifadhi za wanyamapori ili kusaidia kuhifadhi mazingira ya asili na kuengeza mapato kupitia utalii endelevu.
Aidha ameongeza kuwa matika sekta ya afya fedha hizo zitakwenda kusaidia maeneo yote ya huduma za dharura za watoto wachanga ,afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa vijana pamoja na bima ya afya ya pamoja.
“Kwa niaba ta serikali napenda nitoe shukurani kwa serikali ya ujerumani ni waahidi tu serikali tutakwenda kuzisimamia fedha hizi ili kuhakikiaha zinakwenda kufanya yale yaliyokusudiwa”,Amesema
Sambamba na hayo Elijah amezipongeza timu za wataalam kutoka nchi zote mbili kwa kuwezesha majadiliano hayo na hatimie kufikia hatua ya kusainiwa kwa kumbukumbu za majadiliano hayo ambayo zinaelezea ushirikiano wa nchi hizo kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania.
Amesema ahadi zilizotajwa zitasaidia miradi maalumu ikiwemo ya kupunguza migogoro baina ya wanyama na binadamu ambao utagharimu kiasi cha euro milioni tisa na mfumo wa kuomarisha bima ya afya kwa wote kiasi cha Euro milioni tatu.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya Afrika Mashariki wizara ya ushirikiano wa kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani Marcus Von Essen amesema wataendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inaimarika na kuleta tija kwa wananchi wote.