Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah (wa kwanza kushoto) akiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakati kamati hiyo wakiwa katika ziara ya kukagua mradi ya NHC ikiwemo Kawe 711 iliyofanyika leo Machi 20, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi wa jambo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) walipotembelea mradi wa Morocco Square uliopo Jijini Dar es Salaam.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Mhe. Deus Sangu akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara ya kukagua Miradi ya NHC wa Kawe 711, Samia Housing Schem pamoja na Morocco Square.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya NHC.
Muonekano wa mradi wa Morocco Square.
Muonekano wa mradi wa Samia Housing Schem ambapo ujenzi wake unaendeleaje.
Muonekano wa Mradi wa Kawe 711 ambapo ujenzi wake unaendeleaje.
…
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)
imeridhishwa na utekelezaji na usimamizi wa miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa Kawe 711, Samia Housing Schem, Morocco Square, huku wakiadi kuendelea kuishawishi Serikali kuleta fedha ili kumaliza miradi kwa wakati na kuleta tija kwa Taifa.
Akizungumza leo Machi 20, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakiwa katika ziara ya kukagua miradi ya NHC, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Deus Sangu, ameipongeza NHC kwa jitiada za kuendelea kutekeleza miradi kwa ufanisi.
Mhe. Sangu amesema kuwa katika miradi mitatu waliotembelea NHC wamefanya kazi kubwa katika kuhakikisha wametekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
“Majukumu yetu ni kuangalia mitaji ya umma ambayo serikali imewekeza, NHC ni Shirika la kimkakati, mpaka kufikia mwaka wa fedha uliyoisha serikali tayari imewekeza shilingi trilioni 5.14” amesema Mhe. Sangu.
Mhe. Sangu amefafanua kuwa mradi wa Kawe 711 ni mradi wa kimkakati ambapo serikali imewekeza shilingi bilioni 143 ambapo katika utekelezaji wake umefika asilimia 25 na utaratibu kumaliza mwezi Aprili 2026.
Amesema kuwa katika mradi wa Samia Housing Schem serikali imewekeza shilingi bilioni 48 na mpaka sasa nyumba zote 560 tayari zimenunuliwa licha ya mradi bado unaendelea.
Mhe. Sangu ameeleza kuwa kuwa mradi wa Morocco Square una thamani ya shillingi bilioni 137 na tayari umemilika kwa asilimia 98.
“Kamati tunapongeza kwa kazi kubwa iliyofanywa na NHC katika kusimamia na kutekeleza miradi hii ya kimkakati ambayo inatija kwa Taifa” amesema Mhe. Sangu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah, amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassani kwa kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi.
“Kamati imefanya kazi kubwa kutoa taarifa bungeni kuhusu maendeleo ya miradi ya NHC na kusaidia kufikia malengo tarajiwa” amesema Bw. Abdallah.
Amefafanua kuwa mradi Morocco Square una urefu wa ghorofa 17 na unatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni, kwani baadhi maduka yameanza kufunguliwa, huku akieleza kuwa mradi wa Kawe 711 una majengo nane yenye ghorofa 18, nyumba za makazi 422 pamoja na eneo la kuegesha magari na huduma mbalimbali.
Bw. Abdallah amesema kuwa wanaendelea kujenga ushawishi
kwa Serikali kuondoa vikwanzo vyote vinavyozuia watanzania waonaishi ughaibuni pamoja na raia wa Mataifa mengine kushiriki katika uwekezaji kwenye sekta ya Uendelezaji miliki ili kuongeza ufanisi katika utendaji wenye kuleta tija kwa Taifa.
Ametoa wito kwa Serikali kutoa unafuu wa kodi kweny sekta ya vifaa vya ujenzi na kuondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye nyumba za gharama nafuu.
“Tunaendelea kuishawishi Serikali kuanzisha mfuko maalamu wa kusaidia ruzuku kwa nyumba za kisasa za gharama nafuu” amesema Bw. Abdallah.