KILIMANJARO
Paulo Ngiloriti Teveli ambaye alikuwa Mhasibu wa Mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro ametiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 jela bila faini kwa makosa mawili.
Hukumu hiyo imetolewa Machi 19, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Same, mbele ya hakimu mheshimiwa Hellen Hozza, ambapo shauri liliendeshwa na wakili Suzan Kimaro.
Ni kupitia shauri la uhujumu uchumi Na. 23/2022 dhidi ya mshatakiwa huyo.
Aidha,mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa mawili ikiwemo matumizi mabaya ya mamlaka chini ya kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 na kosa la ufujaji na ubadhirifu wa shilingi 8,377,000.
Fedha ambazo zilikusanywa na watumishi watatu wa Hospitali ya Wilaya ya Same.
Fedha hizo ni za makusanyo ya kila siku kutoka kwa wagonjwa ambazo hakuzipeleka benki kwa kipindi cha mwaka 2020.
Pamoja na adhabu hiyo mshatakiwa ametakiwa kurejesha fedha alizofanyia ubadhirifu ambazo ni mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Same.