Na Sophia Kingimali
Mamlaka ya maendeleo ya biashara nchini (TANTRADE) wamepokea msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wao kutoka mamlaka ya biashara ya korea wenye thamani ya zaidi ya bilioni 1.
Akizungumza baada ya kupoke vifaa hivyo Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Latifa Khamis amesema hayo ni matunda mazuri yanayotokana na ushirikiano wa karibu baina ya nchi hizo mbili.
Amesema msaada waliopokea ni pamoja na komputa mpakato( laptop) 10,Desktop 30,vibanda 500,scana 30 pamoja na genereta lenye ukubwa wa kv 60.
“Haya ni matokeo ya ushirikiano wetu tulifanya mazungumzo ya namna ya kuboresha maonesho yetu ili wafanyabiashara wengi zaidi waweze kushiriki na tuwahudumie kwa ufanisi mkubwa na haya ndio matokeo kwani msaada huu hauna masharti yeyote”,Amesema.
Sambamba na hayo Ratifa ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushiriki kwenye maonesho 48 ya biashara ya sabasaba kwani yatakuwa ya aina yake kutokana na vifaa ambavyo wamekabidhiwa kutoka Jamnuhuri ya Corea.
Amesema wadau wa maonesho wamekuwa wakiongezeka wakihitaji kushiriki lakini wamekuwa wakikosa nafasi hivyo kupitia vibanda walivyokabidhiwa watapafa fursa ya kushiriki lakini mapato ya nchi yataongezeka na hatimae uchumi wa nchi kupitia TANTRADE utaweza kuongezeka.
“Maonesho yanayokuja ya 48 ya sabasaba yataimarika na yatakuwa yenye mvuto zaidi hivyo wadau wote msikose kushiriki na tutawahudumia kwa ufanisi mkubwa”,Amesema Ratifa.
Kwa upande wake Barozi wa Jamuhuri ya Corea nchini Kim Sun Pyo ametoa rai kwa Watanzania kuwekeza zaidi nchi Corea kwani kumekuwa na ushirikiano wa karibu baina ya nchi hizo.
Amesema kufutia mazingira mazuri ya uwekezaji na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo wameahidi kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha ufanyaji wa biashara baina ya nchi hizo unaimarika.