Kamishna wa Mamlaka ya Usiamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Bw. Mabula Misungwi akizungumza katika kikao kazi kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Jukwaa ka Wahariri Tanzania (TEF) na Mamlak hiyo kiolichifanyika weye ukumbi wa PSSSF, Ilala jijini Dar es salaam.
Afisa Mawasiliano Mwamndamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Sabato Kosuri akifafanua baadhi ya mambo katika kikao kazi kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Jukwaa ka Wahariri Tanzania (TEF) na Mamlak hiyo kiolichifanyika weye ukumbi wa PSSSF, Ilala jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Maafisa wa uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori TAWA wakiwa katika kikao kazi kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Jukwaa ka Wahariri Tanzania (TEF) na Mamlak hiyo kiolichifanyika weye ukumbi wa PSSSF, Ilala jijini Dar es salaam.
………………………
Ujangili wa wanyamapori, hususan, Tembo umepungia kwa kiasi kikubwa kutokana na uwezeshaji mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyamapori (TAWA).
Hayo yameelezwa na Kamishna wa Mamlaka ya Usiamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Bw Mabula Misungwi, alipokuwa akizungumza katika kikao kazi kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Jukwaa ka Wahariri Tanzania (TEF) na Mamlak hiyo kiolichifanyika weye ukumbi wa PSSSF, Ilala jijini Dar es salaam.
Bw. Mabula amesema ujangili dhidi ya tembo umepungua sana kutokana na uwezeshaji huo ambapo kwa mwma 2020/22 mizoga ya tembo iliyoonenkana katika maeneo yao ni mtatu kutoka mizoga 6.
Amesema tembo ni mnayama muhimu sana katika uhifadhi na kupungua kwa ujangili dhidi yake ni kiashiria cha kuongezeka kwa ulinzi.
Alitaja uwezeshaji huo umesababisha uimarishaji wa ulinzi ulitokana na kungezeka kwa vitendea kazi kama vile magari, ambapo kuna maeneo mengine ambayo hayafifkiki kirahisi hivyo kuongezeka kwa vitendea kazi hivyo kumeimarisha ulinzi.
Pia alitaja kupata uwezeshaji wa teknolojia umerahisha shughuli za TAWA katika ulinzi na uweseshaji huo umeongeza morali na tija kwa wafanyakazi mamlaka hiyo.
Pia amesema kuwa katika kipindi hicho pia migogoro na jamii ilipungua kwa kiasi kikubwa kutokana na uwezeshaji huo. Alisema kuwa kama miigogoro ikipungua shughuli zaulinzi wa wanyamapor zitaimarika kwa kias ikikubwa.
Amesema Migogoro katika mapori ya akiba saba kati ya nane yaliyotolewa maelekezo na Kamati ya mawaziri wa nane wa kisekta imemalizika ambayo ameitaja kuwa ni mapori ya Swgaswaga, Mkungunero, Wamimbiki, Igombe UparambaMpanga Kipengere na Selous na jumla ya vigingi 1681 vimesimikwa kuzunguka mipaka ya hifadhi na eneo la ekari 811.506 limemegwa na kuwapatia wananchi.
Mabula ameongeza kuwa TAWA imeboresha huduma za utalii na kufanikisha ongezeko kubwa la watalii ambapo watalii wa picha waliongezeka kutoka 37.684 mwaka 2020/21 na kufikia watalii 166.964 mwaka 2022/2023 ambapo kwa mwaka 2024 mpaka mwezi februari wameshatembelea watalii 116.529.
Ameongeza kuwa idadi ya meli za kitalii za kimataifa kutembelea eneo la kihistoria la Kilwa imeongezeka kutoka meli 4 mwaka 2020.21 na kufikia hadi meli 8 mwaka 2023/24 na imepelekea ongezeko na watalii zaidi ya asilimia 100waliotembelea kisiwa cha Kilwa Kisiwani.