Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) katika miaka mitatu ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kinajivunia mafanikio kadha wa kadha ikiwemo ongezeko la udahili wa wanafunzi ziadi ya 3800, kutoka wanafunzi 13,0199 mwaka 2021 hadi wanafunafu 17, 084.
Katika ongezeko hilo wanafunzi 105 kutoka nje ya mipaka ya Tanzania, 22 kati yao wanasoma Shahada za Awali na 83 Shahada za Juu huku kwa upande wa watanzania, wanaume 10, 255 na wanawake 6, 829 kati yao wanafunzi 16,023 wanasoma Shahada za Awali na 1, 061 Shahada za Juu.
Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda amesema, ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania limetokana na mashirikiano mazuri, kuimarika kwa Diplomasia, kazi kubwa inayofanywa na Dkt. Samia ndani ya miaka yake mitatu ya uongozi.
Pia ongezeko la mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu pamoja na ufadhili wa wanafunzi kupitia mradi wa wa Samia Scholarship kwa wanafunzi wa Sayansi ikizingatiwa SUA ni moja ya Chuo Kikuu chenye kozi na fani ya Sayansi hapa nchini.
Ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia, SUA imeimarisha mashirikiano na Taasisi za Mataifa mbalimbali kwa uchache, SUA imeingia mkataba wa mashirikiano na Chuo Kikuu cha Artemisa cha Jamhuri ya Cuba makataba utakao saidia kuinua taaluma na ujuzi kwa wataalamu wa nchi hizi mbili.
Mnamo Novemba 17, 2023 SUA ilisaini mkataba wa ushirikiano na Waziri wa nchi wa Masula ya Dunia na mikakati ya Kidiplomasia wa Romania Mhe. Traiana Leurentiu Hristea hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo Romania ilitoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 10 wa kitanzania.
Pia SUA imeingia mkataba wa makubaliano na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) ya kutekeleza mradi wa kudhibiti na kuzuia maambukizi ya magonjwa yatokayo kwa wanyama kwenda kwa binadamu na kutoka kwa binadamu kwenda kwa wanyama.
Katika Mradi huo SUA imejikita katika magonjwa mawili ya Kifua kikuu (TB – Zoonotic Tuberculosis) na ugonjwa wa kutupa mimba ( Brucellosis)
Prof. Chibunda ameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kukiwezesha Chuo kikuu SUA kwa kukipatia fedha kwa jili ya Tafiti mbalimbali ambazo zimekuwa zikitoa majawabu ambayo yanatatua changamoto katika jamii hasa katika Sekta za Kilimoa, Mifugo, Uvuvu na Afya.
“Hivi karibuni watafiti wawili Dkt. Makarius Lalika na Dkt. Ramadhani Majubwa wamepewe fedha shilingi milioni 240 na Serikali ya Dkt. Samia kupitia Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) kwa ajili ya kufanya tafiti. Rais Samia amefanya mambo makubwa sana katika miaka yake hii mitatu hapa SUA” amesema Prof. Chibunda