Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Muleba Mh. Lilian Mwambeleko Machi 15, 2024 ameamua kesi ya Jinai namba 3/2024 iliyokuwa ikiwakabili Bw. Masanja Igolola Afisa Manunuzi VETA, Ndorage pamoja na Denis Rwegalulila Mzabuni.
Mahakama hiyo imewakuta na hatia Bw. Masanja Igolola Afisa Manunuzi VETA, Ndorage pamoja na Denis Rwegalulila Mzabuni na kuwaamuru walipe faini ya shilingi Milioni Moja (1,000,000/-) au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela.
Vilevile, Mahakama hiyo imewataka warejeshe fedha hizo zote TZS 2,800,000/- walizojipatia kwa manunuzi hewa.
Kesi hii ilikuwa kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Bw. Masanja Igolola Afisa Manunuzi VETA, Ndorage pamoja na Denis Rwegalulila Mzabuni.
Wawili hao walishtakiwa kwa kosa la Hongo katika Manunuzi ambapo wanadaiwa kufanya ‘manunuzi hewa’ Mwaka 2019 ya Mashine aina ya Porker Vibrator High F*l na hivyo kujipatia manufaa yasiyo stahiki ya TZS 2,800,000/- ambapo kesi hiyo iliendeshwa na Wakili Kelvin Murusuru
Washtakiwa wamelipa faini ya shilingi 1,000,000/- na kurejesha TZS 2,800,000/- katika ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Muleba.
Wakati huo huo katika Shauri lingine la Rushwa Na. O4$/2024. ambapo Kesi hii pia ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Bw. Raysone Baliyeguje ambaye ni mkusanyaji wa mapato kwa njia ya POS Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Bw. Raysone lishitakiwa kwa kosa la Hongo kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329/2022 kwa kujipatia manufaa yasiyostahili wakati wa ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali TZS 5,292,900/ hivyo kufanya upotevu wa Shilingi 5,292,900/- mali ya Halmashauri ya Muleba. ambapo kesi hiyo iliongozwa na wakili Kelvin Murusuri.
Mahakama hiyo imemhukumu mshitakiwa adhabu ya kulipa faini ya faini ya shilingi Laki tano 500,000/- au kwenda jela miaka miwili na kurejesha fedha zote ndani ya miezi Mitatu.
Mshtakiwa ameenda gerezani akisubiria taratibu za kulipa faini.