Adeladius Makwega-DODOMA
Wakristo wameambiwa kuwa lazima wawe na kiu ya kumuona Mwenyezi Mungu, maana katika ulimwengu wa sasa watu wanakiu na mambo ya kidunia mathalani kusoma ujumbe wa whasaap lakini haya hayasaidii chochote katika kumuona Mungu.
Mtu akiamka tu anakimbilia kuangalia kwenye simu yake kuna nini? Je wewe muumini una kiu ya kusoma neno la Mungu?“Wale Wayunani walikuwa na kiu ya kumuona Kristo, walikuwa na kiu ya kumuona Mungu.
Je Wakristo tuna kiu ya kumuona Mwenyezi Mungu?Je tunakuja kanisani na nia ya kumuona Mungu? Je umuone katika njia gani? Umuone katika sakramenti, Sakramenti gani? Sakramenti ya kumrudia Mwenyezi Mungu.Sisi kama wakristo lazima tuwe na kiu ya kumuona Mwenyezi Mungu, katika hizo Sakramenti zake Sakrament ya Ekaristi Takatifu, Sakramenti ya Kitubio na Sakramenti ya Ndoa.”
Haya yamesemwa na Padri Kenneth Ogoti katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata- Parokia ya Chamwino Ikulu Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma katika misa ya kwanza ya dominika ya 6 ya Kwaresma ya Mwaka B wa Liturjia ya Kanisa.Padri Ogoti akihubiri katka misa ya kwanza ya Jumapili ya Machi 16, 2024 iliyoanza saa 12. 30 ya asubuhi alisisitiza kila muumini kuwa kiu hii ya kumuona Mungu.
Mahubiri haya yalihitimishwa kwa Padri Ogoti ambaye anahudmu katika shule mojawapo ya sekondari ya jimbo hili akinadi kuwa mtu anayeipeda nafsi yake ataipoteza, tusijipende kupita kiasi.Misa hiyo pia iliambatana na nia na maombi kadhaa,
“Utujalie kukubali na kupokea mabadiliko ya maisha yetu- Eee Bwana-Twakuomba Utusikie.”Wakati wa kupokea waaamini walijongea mbele altare huku baadhi yao walijongea katikati ya kanisa hilo, mbele akiwa Frateri na katikati akiwa Padri Ogoti wakikomunishaWakati wa zoezi hilo jirani na alipokuwapo Padri Ogoti muumini mmoja kwa bahati mbaya alipopokea Ekaristi iimponyoka, mara moja Padri Ogorti aliikota na muumini huyu kukomunika, kumbuka ndani ya umbo la mkate ni Yesu mwenyewe.
Hadi misa hiyo inakamilika majira ya saa mbili ya asubuhi, hali ya hewa ya Chamwino Ikulu ni jua la kadli kwa juma zima.