MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM Taifa Mohamed Kawaida amesema jumuiya hiyo imeanza utekelezaji wa kufuatilia fedha za asilimia 30 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa ajili yakutekeleza miradi kwenye Halmashauri zote Nchini.
Kawaida ameyasema hayo wakati akifungua mdahalo wa Seneti ya vyuo na vyuo vikuu,uliofanyika katika ukumbi wa chuo Cha ufundi Ihemi kinachomilikiwa na UVCCM,kilichopo wilayani Iringa Mkoani humo.
Mdahalo huo,umehusisha vyuo na vyuo vikuu nchi nzima ikiwa ni maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu wa viongozi wa Seneti wa vyuo na vyuo vikuu unaotarajia kufanyika hapo kesho machi 16.
Akizungumza Kawaida,aliwataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali ikiwemo sanjari na kueleza kuwa jumuiya hiyo itahakikisha fedha zilizotolewa na Rais asilimia 70 kwa kila Halmashauri Nchini zinawafikia walengwa na kufanya kazi iliyokusudiwa.
Kawaida alisema”hivi karibuni Mhe. Rais amefanya Mambo mawili,moja makubwa ameanzisha mradi wa BBTT ambao unaendelea vizuri katika utekelezaji wake, licha ya changamoto ndogondogo zilizojitokeza katika kutekeleza mradi huo, pia ametoa fedha za asilimia 70 zilizoenda kila Halmashauri zetu Nchini, ambapo asilimia 30 inaenda kwa vijana, wanawake na makundi maalum.