Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa huo Kamishina Jumanne Murilo, akizungumza katika uzinduzi wa Aplikesheni ya usafirishaji abiria inayoitwa Suka App iliyobuniwa na kampuni ya Taksol Limited ya jijini Dar es Salaam kulia ni Luciana Mwambinga Mkuu wa Idara ya Habari Suka.
Naibu Kamishna TRA Bw. Alex Katundu akizungumza katika uzinduzi huo.
Johmathan Kitururu Afisa Leseni LATRA akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Raphael Ndagala Msimamizi wa mifumo ya Tehama Teksol Limited Teksol Limited akizungumza na kuelezea namna Suka App inavyofanya kazi.
…………….
Kampuni ya Teksol Limited iliyoko Jijini Dar es salaam imezindua Suka App maalum kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa abiria ambapo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa huo Kamishina Jumanne Murilo, amewata madereva kuwa waadilifu pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.
Uzinduzi huo umefanyika leo Ijumaa Machi 15, 2024 kwenye Hoteli ya Johari Rutana Jijini Dar es salaam.
Kamanda Murilo amesema kwa kupitia Kampuni zilizopita zinazofanana na Suka App ikiwemo Uba na Bolt miongoni mwa vitu ambavyo vilikuwa vikilalamikiwa na wateja katika uendeshaji wa Kampuni hizo ni tabia za utendaji wa kazi ikiwemo lugha,mavazi, na heshima ambavyo ni miongoni mwa vitu vilivyojenga au kushusha heshima ya kampuni hizo.
“Katika kutekeleza ajira yenu ipo haja ya kufanya mafunzo na kuelekeza jinsi watu watakavyoendesha kampuni katika kutoa huduma sanjari na kutumia lugha zenye staha wakati wa kuwahudumia watu”, amesema Kamishina Murilo
Amesema kampuni zinazotoa huduma ni wadau muhimu sana kwa Jeshi la Polisi na Serikali kwenye masuala ya kiusalama licha ya watu hao kupata kazi wao kama Jeshi wanatarajia kuwa nao karibu sana kama sehemu yao ya tatu ya jicho ya masuala ya kiusalama.
Aidha,ameitaka Kampuni ya Teksol kutoa ajira kwa watu ambao wanamsaada siyo tu kwa faida yao bali kwa faida ya Mkoa wa Dar es salaam na Taifa kwa ujumla.
Kwaupande wake Msimamizi wa mifumo ya Tehama Kampuni ya Teksol Limited Raphael Ndagala, amesema faida za kutumia Suka App ni usalama wa uhakika na bei.
“Kumekuwa na mfumuko wa bei katika kutumia usafiri huu mara bei inaongezeka bila utaratibu maalumu hivyo unapotumia huduma yetu unaweza kufuatilia gharama zako na kujua umetumia kiasi gani”, amesema Ndagala.
Amesema suala la usalama tunalizingatia sana kutokana na kuwepo tabia za madereva kutofuata sheria za barabarani hivyo wao kama Suka App wamekuja na utaratibu wa kuhakikisha dereva anaekiuka sheria anawajibishwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria hususani madereva pikipiki na bajaji.
Naye Afisa Leseni kutoka Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) Jonathani Kitururu, amesema kupitia kanuni za LATRA za usafiri wa kukodi za mwaka 2020 kanuni ya 18 ndio iayozungumzia Tax mtandao na unatoa mashariti ili Kampuni iweze kutoa huduma ni lazima wasajiliwe.
“Pia kanuni za LATRA zinatoa masharti kadhaa ikiwemo upatikanaji wa mfumo muda wote,kutoa taarifa sahihi kwa wakati pamoja na mtoa huduma aliesajiliwa kutoruhusiwa kutoa huduma kale ambapo leseni yake imemaliza muda wake”, amesema Kitururu
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Naibu Kamishina kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alex Katundu, amesema uwepo wa huduma hiyo ni kigezo cha ukuaji wa uchumi ndani ya nchi.
“Kuongezeka kwa wadau wa uwekezaji kama Suka App ni Imani yangu kuwa tutaendelea kuwavutia wawekezaji kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi hatua itakayosaidia kukuza uchumi wetu”, amesema Katundu.