Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akizungumza jambo wakati akifungua Kongamano katika Kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Mlaji Duniani iliyofanyika leo Machi 15, 2024 katika Hotel ya Protea, Upanga Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Ushindani (FCC) Dkt. Aggrey Mlinduka akizungumza jambo wakati akifungua Kongamano katika Kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Mlaji Duniani iliyofanyika leo Machi 15, 2024 katika Hotel ya Protea, Upanga Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw. William Erio akizungumza jambo wakati akifungua Kongamano katika Kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Mlaji Duniani iliyofanyika leo Machi 15, 2024 katika Hotel ya Protea, Upanga Jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akizungumza jambo wakati akifungua Kongamano katika Kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Mlaji Duniani iliyofanyika leo Machi 15, 2024 katika Hotel ya Protea, Upanga Jijini Dar es Salaam.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika Kongamano la Kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Mlaji Duniani.
Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Ushindani (FCC) Dkt. Aggrey Mlinduka, Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw. William Erio, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt. Eliezer Feleshi wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika Kongamano la Kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Mlaji Duniani.
………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema Serikali kupitia Mamlaka zake zitaendelea kuweka utaratibu wa kuthibiti watao huduma watakaotumia mfumo wa Teknolojia wa akili mnemba (artificial intelligence) jambo ambalo litasaidia kuwalinda walaji au wateja nchini.
Akizungumza leo Machi 15, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kongamano katika Kilele Cha Maadhimisho ya Siku ya Mlaji Duniani, Dkt. Hashil Abdallah, amesema wadau wote wanapaswa kujipanga vizuri kama Taifa ili kunufaika na fursa zinazotokana na teknolojia katika kutoa huduma bora kwa jamii.
Dkt. Abdallah mesema kuwa matumizi ya akili mmemba ni dhama mpya ambayo imeshika kasi duniani kote hivyo ni jambo la umuhimu kwa vyombo vya usimamizi vya utendaji wa uchumi wa soko vinavyotoa huduma kwa wananchi kusimamia ikiwemo Tume ya Ushindani (FCC).
“Akili mmemba imekuwa ikitumika sehemu mbalimbali kwa kutoa huduma katika mazingira rafiki na haraka ikiwemo usafirishaji wa abiria bila uwepo wa dereva” amesema Dkt. Abdallah.
Amesema kuwa ili kuwezesha kupatikana wa uthibiti na uhakika wa matumizi ya akili mmemba katika kutoa huduma kwa walaji au wateja ni muhimu kuzingatia uwajibikaji, haki na mslahi ya walaji hasa kuwalinda mlaji katika uchumi wa soko nchini.
“Tunapaswa kuhoji na kufanya tafiti ya namna ambavyo mifumo hii inaundwa na kusimamiwa, hayo yakifanyika kwa kuzingatia mslahi ya mlaji itasaidia kufikia malengo” amesema Dkt. Abdallah.
Amesisitiza umuhimu wa kubainisha hasara na faida za matumizi ya akili mmemba ili kuwezesha watunga sera, sheria, mifumo ya usimamizi, uthibiti pamoja na utafiti ili kuthibitisha faida au hasara zilizopo.
Dkt. Abdallah amesema kuwa wakati umefika wa kuangalia namna bora ya kuelimisha jamii kuhusu kutatua changamoto za mfumo huo ili wawe makini katika matumizi ya teknolojia hiyo.
“Sisi sote tunamatarajio ya kuraisisha utoaji wa huduma kwa ubora zaidi kwa walaji kwa kutumia Teknolojia kwa nyenzo muhimu kwa ustawi na mslahi ya walaji na uchumi kwa ujumla” amesema Dkt. Abdallah.
Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Ushindani (FCC) Dkt. Aggrey Mlinduka, amesema kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia matumizi ya akili mnemba hayakwepeki katika duniani ya Sasa.
Dkt. Mlinduka amesema kuna kila sababu ya kutoa mafunzo endelevu kwa wasimamizi wa kisekta ili kuhakikisha walaji hawapati madhara katika matumizi ya akili mnemba.
“Ipo haya kwa serikali kukabiliana na matumizi ya akili mnemba katika mifumo ya kisera, sheria pamoja na na kuweka mikakati ya ulinzi” amesema Dkt. Mlinduka.
Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw. William Erio, amesema kuwa katika kuadhimisha siku ya mlaji duniani wameendelea kutoa elimu kwa jamii na kupokea changamoto kwa ajili ya kuzifanyia kazi.
Bw. Erio amewashukuru wadau wa mbalimbali wa maendeleo kwa ushirikiano ambao umewasaidia kufanikisha utekelezaji wa majukumu yao ili kuleta tija kwa Taifa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, amesisitiza umuhimu wa kuwa bajeti ya kutosha ambayo itasaidia FCC pamoja na Baraza kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta tija katika sekta ya uchumi nchini.
Dkt. Feleshi amesema kuwa ili kupatikana kwa uelewa mkubwa inatakiwa kufanyika kwa tafiti na kujua matokeo ya kila siku kitu ambacho litasaidia kupata haki ya walaji.
Kongamano hilo limejuimuisha wadau mbalimbali ikiwemo TEHAMA, Vyuo Vikuu, Taasisi za Utafiti, Afya, Sera, Sheria pamoja na Wafanyabiashara kutoka Sekta mbalimbali nchini kwa ajili ya kujadili dhana ya akili mmemba kwa na kuangalia namna ya kumlinda mlaji dhidi ya changamoto zinazoweza kujitokeza.