Na Joel Maduka, Geita
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa MNEC Chacha Wambura(WAJA) amekabidhi Baiskeli Hamisini kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ambayo aliitoa kwenye Baraza la wazazi ambao waliomba baiskeli hizo kwa nia ya kuwafikia wanachama kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuendelea kufuatilia uhai wa chama kwenye mashina.
Akikabidhi Baiskeli hizo MNEC Chacha amesema ametekeleza ahadi hiyo ya kutoa baiskeli ni kufuatia maombi ya Baraza la wazazi ambao waliomba Baiskeli Hamsini kwaajili ya kuwapatia viongozi wa jumuiya hiyo kwa lengo la kusaidia uhai wa chama na jumuiya
“Kuna siku ya Baraza la wazazi walinialika kama mngeni rasmi ambapo waliomba kuwasaidia baiskeli ambazo zitawafikia Wanachama wa urahisi zaidi ni kweli nililichukua suala hilo lakini mbali na baiskeli pia tumesaidia upatikanaji wa pikikipiki ambazo zitasaidia kwenye jumuiya ya wazazi lakini mbali na Baiskeli pia tulitoa Kompyuta na Mashine ya Photocopy na kusaidia maitaji muhimu ya kumaliza Nyumba ya Katibu”Chacha Wambura MNEC.
“Lakini pia Mhe ,Mwenyekiti wa wazazi Taifa mbali na kutoa Baiskeli hizi kwa wazazi bado tumehaidi kuzifikia jumuiya zingine hili pia nazo ziweze kupata Baiskeli nia yetu ni kutaka kuona jumuiya zetu ndani ya chama zinakuwa imara na zinaendelea mbele zaidi kimaendeleo” Chacha Wambura MNEC.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Fadhili Maganya amemshukuru MNEC Waja kwa kutoa Baiskeli hizo huku akisisitiza kwa viongozi ambao watapatiwa ni vyema wakaenda kuzitumia kwa matumizi sahihi ambayo yamepangwa na sio matumizi yao Binafisi.
“Najua tumeanza kutoa pia Pikipiki kwa Mikoa yetu na Mkoa wa Geita zitafika lakini niwaombe viongozi ambao mtapatiwa hakikisheni mnazitunza Baiskeli na Pikipiki tutakazowapa na ni vyema mkatambua sio mali zenu ni mali za chama hivyo msitumie kwa matumizi yenu binafisi” Fadhili Maganya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa.