MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ya Taifa na Mlezi wa UVCCM vyuo na vyuo vikuu Tanzania, Mohammed Ali Kawaida amewasihi vijana Nchini kuacha kutumika kwa mwamvuli wa ahadi za ajira, kwani tatizo la ajira ni la Dunia nzima na sio Tanzania pekee.
Kawaida ameyasema hayo mkoani Iringa leo hii machi 14/2024 wakati akizungumza na viongozi wa UVCCM Seneti vyuo na vyuo vikuu katika ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa.
Kawaida amekemea vitendo vya wanasiasa kuwatumia vijana ili kusukuma ajenda zao na kujinufaisha.
“Vijana amkeni, msikubali kutumika kusukuma ajenda za watu ili waweze kufanikisha mambo yao kwa maslahi yao binafsi,Serikali yenu ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuchukua jitihada mbalimbali kuhakikisha vijana mnapata mikopo ili muweze kujikwamua kiuchumi” – Amesema Kawaida.