Mwezeshaji wa mafunzo ya mapitio ya sheria za habari Hawra Shamte akiwafafanua juu ya sheria ya Makosa ya Mitandao kwa wandishi wa habari Kisiwani Pemba kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika kwenye ukumbi wa TAMWA
Wandishi wa habari Kisiwani Pemba wajidali jambo kuhusiana na sheria ya Makosa ya Mitadaoni kwenye mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na TAMWA (picha na Masanja Mabula ).
Na Masanja Mabula ,Pemba.
WAANDISHI wa Habari Kisiwani Pemba wamesema uhuru wa habari bado unabinywa na uwepo na sheria kandamizi zinazowanyima fursa ya kuleteleza majukumu yao ya kila siku kwa uwazi na weledi.
Miongoni mwa sheria ambazo ni kikwazo kwa wandishi wa habari ni sheria ya Makosa ya Mitandao NO 14 ya mwaka 2015.
Sheria hii imebainika kuwa na mapungufu ambayo kama haijafanyia marekebisho inaweza kuviza na kudumaza uhuru wa habari na kuwanyima fursa wandishi ya kuihabarisha jamii kama iliyoanishwa kwenye katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 , Ibara ya 18 . (2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbali mbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii
Katika Ibara ya 23: Unyayasaji wa kupitia mtandao (cyber bullying) haujapewa maana. Sheria inatakiwa kuweka bayana maudhi ya kihisia ni nini. Kwani mtu yeyote atakayeudhiwa ‘kihisia’ au kudai kuwa hisia zake zimeudhiwa anaweza kushtaki.
Aidha Sio kila linalosababisha maudhi ya kihisia ni unyanyasaji Ibara ya 27: Ni nani anaamua kitendo fulani ni kula njama? Mazungumzo ya kawaida na maamuzi ya kukubalika na upande mmoja yanaweza kutafsiriwa kama kula njama na watu wa upande mwingine.
Na katika Ibara ya 31 (3a): Sheria ya kiingereza inasema ‘as soon as practicable’ lakini ya Kiswahili inasema wakati wa upekuzi na ukamataji wa mali. Hizi zina maana tofauti. Ibara hii inawapa mamlaka Wakuu wa Vituo vya Polisi kufanya upekuzi na kuchukua mali(za kielektroniki) na taarifa binafsi za raia bila amri ya Mahakam.
Hivyo walishauri sheria hii kufanyiwa marekebisho hasa katika Ibara tajwa hapo juu ili kuweza kukuza uhuru wa habari na kuwawezesha wandishi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi .
Pia mapungufu mengine ni katika Ibara ya 16: kinachozungumzia suala la ukweli, uongo au upotoshaji,
Swlai ni kwamba ni nani ana mamlaka ya kubainisha kuwa jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la UKWELI, UONGO au UPOTOSHAJI? Ni wazi kuwa mamlaka husika inaweza tumia hili kama mtego kwa manufaa yao.
Kipengele hiki kama vingine kimeambatanisha muda usiopungua bila kusema muda usiozidi. Hivyo mtuhumiwa anaweza kufungwa hata kifungo cha maisha kutokana na mamlaka ya mahakama.
Watu binafsi wanaweza kutumia vibaya kifungu hiki kuzuia uhuru wa maoni kwa kuwaburuza watumiaji wa mtandao mahakamani kila kukicha na kuwapotezea muda wahusika ambao wanaweza kubainika mwishoni kuwa walionewa.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Hawra Shamte aliwataka kuendelea kuzisoma sheria na kuzielewa ili wasije wakaingia kwenye matatizo na mamlaka husika.