*Binadamu kwenye kila utakachofanya ana majibu ya pande mbili
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 12, 2024 ametoa rai kwa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi Rehema Madenge ambaye amehamishiwa Ruvuma na Katibu Tawala mpya wa Mkoa huo Dkt Toba Nguvila pamoja na watumishi wengine wakati wa Kikao cha kumuaga Katibu Tawala huyo na kumkaribisha Katibu Tawala mpya katika ukumbi wa Anatoglo Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam
Akiongea katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Kamati ya usalama ya Mkoa, Wakuu wa Taasisi na Mashirika yaliyoko katika Mkoa huo pamoja na Viongozi wa CCM Mkoa, RC Chalamila amesema ” Fanyeni kazi kwa nguvu zote kwa kujiamini bila kuogopa chochote binadamu siku zote anamajibu ya pande mbili ukifanya vizuri ana jibu na usipofanya vizuri anajibu pia” Leo uko Mkoa wa Dar es Salaam utasifiwa sana siku ukihamishwa binadamu yule yule utasikia tulijua tu hawezi yule…Alise RC Chalamila
Aidha aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi Rehema Madenge amesema mabadiliko ndio Utumishi amewashukuru watumishi wote katika Mkoa huo kwa ushirikiano wao katika Kipindi chote akiwa DSM ana anawakaribisha sana Ruvuma.
Naye Katibu Tawala mpya Dkt Toba Nguvila amebisha hodi katika Mkoa huo ambapo amesema kikubwa anachokiomba ni ushirikiano ili kuweza kuwahudumia wakazi wa Dar es Salaam na Taifa kwa Ujumla.
Mwisho kwa niaba ya Kamati ya Usalama ya Mkoa Afande Jumanne Muliro amemshukuru RAS Madenge kwa malezi na ushauri wake kwa kamati ya usalama ya Mkoa ambapo amesema ni imani yake kuwa Katibu Tawala mpya Dkt Toba Nguvila ambaye amepokea kijiti ataendelea vema kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.