Aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi Rehema Madenge ambaye kwa sasa ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma amekabidhi rasmi Ofisi kwa Katibu Tawala mpya Dkt Toba Nguvile ambaye amehamia kutoka Mkoa wa Kagera kutokana na mabadiliko ya hivi karibuni yaliyofanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo amewashukuru watumishi wote wa Mkoa huo kwa kumpa ushirikiano katika Kipindi chote alichokuwa akihudumu katika Mkoa huo ambapo amewaomba kuendelea kumpa ushirikiano Katibu Tawala mpya Ndg Dkt Toba Nguvile.
Kwa upande wa Dkt Toba Nguvile amewahakikishia watumishi wa Sekretariati ya Mkoa wa Dar es Salaam kuendeleza yote ya mtangulizi wake na kuibua mapya ambapo ameahidi ushirikiano wa kutosha katika Kipindi chote cha uongozi wake Ofisi yake iko wazi wakati wote mwenye ushari, mawazo ya kujenga, anakaribishwa.
Aidha makabidhiano hayo yamefanyika leo machi 12, 2024 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ilala Boma.