Na Sophia Kingimali
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steven Mengere ametoa rai kwa wanasiasa na wanaharakati nchini kufanya harakati na siasa za hoja na sera pasipo kumdhalilisha mtu mwingine.
Hayo ameyasema leo wakati wakati akizungumzia mikakati ya taasisi hiyo lakini pia miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake
Amesema wamekuwa kwa mwaka huu wa 2024 wamejipanga kushirikiana na watu wa makundi mbalimbali wakimemo walemavu ambao wamekuwa wakisapoti juhudi za Rais Dkt Samia.
Amesema katika kusheherekea miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia wameandaa tamasha kubwa ambalo watashirikiana vijana wa bodaboda na watu wenye ulemavu pamoja na kutoa mahitaji mbalimbali kwa watu wenye uhitaji lakini pia kufanya Dua ya pamoja kwa ajili ya kuwaombea viongozi waliotangulia mbele ya haki na wananchi kwa ujumla.
Sambamba na hayo Mengere ametoka rai kwa wanaharakati na wanasiasa kufanya siasa za hoja na sera na si kutumia lugha za matusi na udhalilishaji lakini pia kutumia mitandao kutangaza biashara na vivutio vya nchi.
“Sisi kama taasisi hatutavumilia matusi na kejeli kwa Rais wetu nitoe rai tutumie mitandao hii ya kijamii kutangaza biashara lakini pia vivutio vyetu lakini sio kutafuta kiki kwenye mitandao kwa kuonyesha maisha ambayo si yako”Amesema.