Dodoma
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Wa Idara ya Habari-Maelezo Bw. Mobhare Matinyi amevipongeza vyama vya Maofisa Uhusiano na Mawasiliano Tanzania ( PRST) na Chama cha Maofisa Uhusiano na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa mapendekezo ya kuwa na Sheria itakayosimamia taaluma ya Uhusiano na umma(PR) na Mawasiliano nchini.
Bw. Matinyi ameyasema hayo leo wakati wa kikao cha pamoja wa viongozi wa vyama hivyo kilichofanyika kwenye ofisi za Maelezo jijini Dodoma.
“Nawashukuru kwa taarifa hii na nimeona yote yaliyopendekezwa ni mazuri kwa tasnia Uhusiano na Mawasiliano nchini”.
“Nimefurahi pia kuona vitu vingine mlivyopendekeza vinafanana na nchi nyingine ambazo tunafanana nazo kimazingira na mengine ambayo ni msingi kwa nchi na kwa Africa Mashariki.
Ameongeza kusema kwamba eneo la Mawasiliano na Uhusiano lilikua halina nguvu, na kwasasa ambapo Dunia imebadilika, Mawasiliano ni eneo muhimu sana kupewa kipaumbele. Pia, amepongeza jitihada za ushirikiano baina ya vyama vya kitaaluma ya Uhusiano na Mawasiliano kwa kuunda East Africa Public Association (EAPRA) kama chombo kitakachosaidia Jumuiya yetu kwenye masuala ya Mawasiliano na Uhusiano(PR).
Hata hivyo amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kulichukua jambo hilo na ahadi yake ya kuunda kamati ya kuliendeleza na kulifanyia kazi.