Mbunge wa jimbo la Lindi Mjini Hamida Mohammed Abdallah amekabidhi kilo 1000 za unga wa mahindi kwa kaya 82 zilizopo mitaa ya Kumbaila, Livengula na Mapokezi katika kata ya Ng’apa Manispaa Lindi ambao makazi yao yameingiliwa na maji na mengine yakibomoka.
Akizungumza wakati alipowatembelea na kutoa misaada hiyo Mbunge Hamida alisema tayari hatua za haraka zimekwisha chukuliwa ikiwemo kuwasiliana na mamlaka husika ili waweze kushughulikia tatizo la mto Lupululu ambao unasababisha adha hiyo sambamba na kulifikisha katika ya ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia mazingira.
Katika hatua nyingine Mbunge amepita kuwafariji na kuhani msiba wa mwanachama wa Ccm na kutoa pole kwa wafiwa na kuwaomba kuwa wavumilivu kipindi hichi kigumu wanachopitia.
Lakini pia ametembelea mkulima wa Nazi ng’apa bwana Abdeleheman Chapapa.
Wakazi wameshukuru mbunge kwa kuja kuwafariji na kwa msaada huo aliowaletea na kuomba kuongezwa zaidi kwa nguvu katika kupambana na kukabiliana na changamoto hizo za maji